Waziri wa Afya Ustawi
wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amewataka wazazi na
walezi kushirikiana na Serikali katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji
wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto nchini .
Hayo ameyasema katika
Nyumba ya kulelea Wazee, Welezo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya matumizi
mbali mbali kwa ajili ya nyumba salama ya kuhifadhia wahanga wa udhalilishaji
kutoka kwa Muakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji Nchini
Tanzania (IOM) Dr Qasim Sufi .
Amesema vitendo vya
udhalilishaji ni janga la kitaifa hivyo iko haja jamii kiujumla kushirikiana
kwa pamoja na Serikali ili kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka katika jamii .
Aidha ameitaka jamii
kutokuwa na muhali wa kuwaficha wahalifu wa vitendo hivyo kufanya hivyo
kutasaidia mapambano ya vita dhidi ya udhalilishaji .
“Ni wajibu wetu
kushirikiana kwa pamoja kuunga mkono mapambano ya vita dhidi ya
udhalilishaji wa wanawake na watoto tuacheni muhali, tuwe mstari wa mbele kwa
kutoa ushahidi wa ukweli .“alisema Waziri .
Nae Muakilishi Mkaazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji Nchini Tanzania (IOM) Dr Qasim
Sufi amesema iko haja kusaidia nyumba salama hapa Zanzibar kwa lengo la
kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji .
Amesema tatizo hilo ni
la kidunia ambalo limekuwa likiwaathiri hususan wanawake na watoto ambao
wameonyesha kuathirika zaidi duniani kote.
Kwa upande wa
Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee, Abdalla Saleh Omar amesema
nyumba salama inapokea watoto waliofikwa na kadhia mbali mbali ikiwemo
udhalilishaji wa kingono kama kubakwa, kulawitiwa pamoja na kupigwa
kupitiliza .
Pia amesema
usafirishaji haramu wa wahanga ambao hutumika kwa kufanyakazi za
majumbani wakiwa katika umri mdogo hupatia hifadhi ya muda watoto hao, ambapo
kwa kipindi cha mwezi wa Agosti hadi Oktoba mwaka huu wahanga walipokelewa 22
katika nyumba salama kwa hifadhi ya muda.
Hata hivyo alisema
wahanga hao wa kike ni 19 na wa kiume ni 3 wengine hupelekwa katika
nyumba salama kwa shaka ya kudhurika ikiwa wazazi wakishtukiwa kuwa watumiaji
wa madawa ya kulevya pamoja na watoto waliokosa jamaa hapa Zanzibar .
0 Comments:
Post a Comment