Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa wito huo alipojumuika pamoja
katika mazoezi na wanavikundi vya mazoezi Zone “A” katika uwanja wa
Maisara jijini Zanzibar.
Mhe. Hemed alielezea
kufurahishwa kwake kwa kuona muako wa wazanzibari katika kufanya mazoezi kuwa
mkubwa jambo ambalo litasaidia kupunguza wagonjwa wa maradhi mbali mbali ikiwemo
presha na kisukari.
Aliwataka wananchi
kutenga muda maalum wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuushughulisha mwili ili
kuichangamsha akili na kuepukana na athari zisizokuwa za lazima.
Alisema ni jambo la
kufurahisha kuona makundi ya Rika mbali mbali, ikiwemo vijana, watu wazima na
kina mama kutenga muda wao kwa kushiriki mazoezi hayo, jambo ambalo linaleta
faraja kuwa jamii imefahamu umuhimu wa kufanya mazoezi kila siku.
Sambamba na hayo Mhe.
Hemed alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dr Mwinyi
imedhamiria kuleta hamasa katika michezo, ikiwemo suala la mazoezi ya
viungo, hivyo ni vyema kwa wanamichezo hao kutumia fursa hiyo kuweza
kujiendeleza zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa chama cha wafanya mazoezi ya viungo Zanzibar Said Suleiman Said alimueleza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa
Nae, katibu wa ZABESA
Suleiman Yussuf Sitwale alieleza kuwa Zone A ina jumla ya vikundi 12 ambapo
inajumuisha vikundi vilivyopo kuanzia Serena hadi mazizini, ambapo wamemuomba
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa mlezi wa Ukanda huo.
Alileza kuwa, Mazoezi
hayo ni matayarisho ya siku ya mazoezi ya viungo Januari 01 ya kila mwaka
ambapo kwa mwaka huu wanategemea kupokea wageni zaidi ya 400 kutota Tanzania
bara.
0 Comments:
Post a Comment