MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman,
amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya juhudi kubwa
kusimamia maslahi ya Watu wenye Ulemavu katika nyanja tofauti kwa nia ya
kutoa fursa zaidi za maendeleo ikiwemo suala la elimu ya kuwajengea uwezo
mkubwa zaidi.
Othman ameyasema hayo leo huko Nungwi Wilaya ya Kaskazini
‘A’ Unguja alipozungumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya watu wenye
ulemavu duniani ambazo kitaifa zimeadhimishwa leo hapa Zanzibar.
Makamu amesema kwamba kupitia wizara ya Elimu ya Zanzibar,
Serikali imeanzisha mfumo wa shirikishi na mjumuisho wa elimu ili kuwapatia
fursa kubwa za stadi za maisha sambamba na kutoa nafasi za ungozi kwa watu
wenye ulemavu Zanzibar wa waina mbali mbali .
Amefahamisha kwamba katika jitihada za kuendelea kutoa fursa kwa
watu wenye ulemavu hivi karibu ni serika.li ya
mapinduzi ya Zanzibar itaanzisha ujenzi wa shule maalum jambo ambalo linaongeza
juhudi katika kuongeza mslahi ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Aidha amesema kwamba serikali imeimarisha mazingira bora ya
kusaidia na kushajiisha washirika wa maendeleo ili kuwasaidia zaidi Watu
Wenye Ulemavu jambo ambalo linakwenda sambamba na juhudi za dunia za kuwatetea
watu wenye ulemavu kupitia maazimio mbali mbali ambayo yanaongeza
nguvu katika kuingiza masuala ya watu wenye ulemavu katika masuala tofauti ya
nchi.
Amesema Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuiya ya
kimataifa inaendelea na michakato mbali mbali ya kuimarisha sera na
sheria zinazosimamia maslahi ya Watu wenye ulemavu, jambo ambalo limesaidia
sana kuanzishwa kwa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar chombo ambacho
nimuhimu katika kusimamia na kutetea haki zao.
Amesema kwamba serikali inajitihadi kuwa na sheria bora za
kulinda maslahi ya au wenye ulemafu pamoja na kuweka mkazo mkubwa wa usimamizi
wake ikiwa ni pamoja shuriki wa watu wenye ulemavu katika masuala ya siasa
katika kuweka ushirikishwaji sawa kama haki yake ya kisiuasa sambamba kujengwa
miundo mbinu rafiki kwa jamiii hiyo ili Zanzibar kuwa nchi ya mfano katika
kulinda maslahi ya watu wenye ulemavu.
Aliwakumbusha Baraza , Viongozi na Jumuiya ya watu wenye ulemavu
Zanzibar kujaandaa kuhesabiwa katika sense ijayo ya mwaka 2022 ambayo itasaidia
kupaanga masuala mbali mbali ikiwemo maslahi ya watu wenye ulermavu .
Aidha aliwakumbusha kinamama kwenda hospitali mapema kuchunguzwa
afanya za watoto na wale ambao watakuwa wamepata watoto wenye ulemavu atrhari
za ulemavu zitaweza kupunguzwa iwapo wamewahishwa hospitali.
Pia Mhe. Othman amewataka wanajamii kuacha tabia iliyojengeka ya
kusbabaisha ongezeko la ajali kwa ajali za barabarani zinazotokana na uzembe
kwa kutozingatiwa ipasavyo kanuni na sheria za usalama barasbarani.
Naye Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar Dk Saada Salum Mkuya Salum amsaema kwamba takwimu zinaonesha kuwa
Zanzibar inaasilimia 5.8 ya watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali na
takwimu hizo zinaoweza kuongezeka kwa kuwa watu wengi hawajajitokeza na taarifa
zao kufahamika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud
amsema kwamba mkoa huo ulitajwa kwamba ulikuwa unaongoza katika takwimu za
vitendio vya udhalilishaji lakini hivi sasa hgali hiyo imekuwa na mabadiliko
makubwa .
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu
Zanzibar Bibi Salma Saadat, amepongeza juhudi za serikalki katika kuhakikisha
maslahi ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa na kulindwa vyema na kuwataka
wanajumuiya hizo kuhakikisha wanaongeza ushirikiano katika kudai haki zao mbali
mbali.
Siku ya watu wenye ulemavu duniani huadhimishwa kila ifikapo
Disemba tatu ya kila mwaka ambapo Ujumbe wa mwaka huu ni “Uongozi na
Ushirikishwaji wa Watu wenye ulemavu kuelekea ujumuishwaji na ufikiwaji
endelevu baada ya uviko 19
0 Comments:
Post a Comment