Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Ustawi wa
Jamii imetunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza ya uandaaji wa taarifa za hesabu
chini ya viwango vya IPSASs, katika kundi la vyuo vya elimu ya juu nchini kwa
mara ya tatu mfululizo.
Akizungumza baada ya
kupokea tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Mkuu wa
Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni amesema ni furaha sana kupata tuzo
hiyo kwa mwaka mwingine kwani imewafanya kubaki kwenye viwango vya ubora katika
utunzaji wa hesabu.
Dkt. Joyce Nyoni
ameongeza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuhakikisha inasimamia matumizi ya fedha
za Serikali zinazotolewa hasa katika kutekelza miradi mnalimbali ya maendeleo
katika Taasisi hiyo.
“Na leo hii
baada ya kuongeza juhudi tumepata tuzo ya mshindi wa kwanza ya taarifa ya
hesabu ya mwaka 2020 na tunajipanga kuendelea kushika nafasi hii ya kwanza bila
kushuka chini’’ alisema Dkt. Joyce.
Aidha Dkt. Joyce
amewapongeza watendaji na wafanyakazi wote wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutukeleza
majukumu yao na kuwezesha kupata tuzo hiyo amnbayo imeewapa heshima na
kuaminiwa na Serikali na umma kwa ujumla katika matumizi mazuri ya fedha.
“Naomba tuendelee
kushirikiana kwa pamoja, tuendelee kufanya kazi kwa uweledi kwasababu tumekuwa
tukifanya hivyo, ndio maana tumepata tuzo hii wote kwa pamoja. Tuzo hii ni yetu
Taasisi wote kwa pamoja’’, alisema Dkt. Joyce.
Dkt. Joyce
amefafanua kuwa tuzo hizo zina tija sana katika kuipa Serikali imani na Taasisi
zake ili kuihakikishia fedha zinatumika vizuri na kama zililivyokusudiwa katika
shughuli mbalimbali katika Taasisi mbalimbali za Serikali.
Kwa upande wake
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii CPA Athuman Senzota amesema tuzo
hizo zina maana sana kwasababu zinaipa Serikali imani na na inaonesha kwamba
utawala bora lazima uendane na hesabu ambazo watu wengine waweze kuzisoma na
kuelewa.
Taasisi ya Ustawi wa
Jamii inachukua tuzo hii kwa mara sita mfulilzo, ikiwa imeshachukua tuzo hii
mara mbili katika nafasi ya mshindi wa pili, mara moja katika nafasi ya mshindi
wa tatu na mara tatu katika nafasi ya mshindi wa kwanza. Kila mwaka Bodi ya
Uhasibu Tanzania hutoa tuzo hizo kwa Taasisi za umma na binafsi zilizoshiriki
katika kinyang’anyiro hicho.
0 Comments:
Post a Comment