Timu ya soka ya Zimamoto imetoka kidedea mbele ya KVZ kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa Mao Zedong.
Bao hilo la pekee ambalo limewafikisha pointi 15 liliwekwa kimiyani na mchezaji wao Suleiman Ame Uwesu.
Kwa ushindi huo Zimamoto imepanda hadi nafasi ya tano kutoka wa nane katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KMKM wenye pointi 20
Huko katika uwanja wa Gombani Pemba Kisiwani imefungwa bao 4-0 na Machomane.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho ambapo katika uwanja wa Amaan saa 10:00 Uhamiaji itacheza na Polisi na saa 1:00 usiku JKU itapambana na KMKM, wakati katika uwanja wa Mao Zedong Black Sailor. itacheza na Kipanga.
Aidha katika uwanja wa Gombani Pemba Yoso Boys itacheza na Mafunzo saa 8:00 mchana na saa 10:00 Mlandege itacheza na Selem View.
0 Comments:
Post a Comment