Mkurugenzi
wa Chama cha Waandishi wa Wanawake Tanzania, Zanzibar ( TAMWA, ZNZ) DK. Mzuri Issa Ali amesema Vyombo vya habari
vina nafasi kubwa ya kuweka usawa wa
kijinsia katika nafasi za uongozi kwa wanawake.
Dk.
Aliyaeleza hayo Huko Tungu Mkoa wa Kusini Unguka katika afisi ya Tamwa, wakati akifungua mkutano wa uwandishi wa habari na wadau kutoka taasisi za habari na tasisi
zinazoshughuika na utetezi wa wanawake ambapo kuliwasilishwa kwa ripoti ya Utafiti
jinsi vyombo vya habari vinavyoripoti
habari za wanasiasa wanawake hapa nchini.
Alisema
umefika wakati sasa vyombo vya habari kuandika habari ambazo zinaeleza umuhimu wa
wanasiasa mwanamke katika majukumu yao ya
uongozi na pia kuelezea yale mazuri ambayo wanayoyafanya katika utendaji
wao.
“Tukiandika
habari za utendaji wa wanawake na umuhimu wao wa kushika uongozi katika siasa
italeta hamasa kwa wanawake wengine kuingia
katika kugombania nafasi mbalimbali za uongo hizo” alisema Dr. Mzuri
Alisema
lengo la kufikia 50 kwa 50 litaweza kufanikiwa ikiwa vyombo vya habari
vitajikita katika kuandika habari za wanawake ambazo zitawatia hamasa za
kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi zote.
“Masuala
ya uongozi ni matakwa ya Kitaifa na kimataifa mpaka 2030 tuwe tumefikia asilimia 50 kwa 50” alisema Dr. Mzuri.
Akiwasilisha
Utafiti huo uliofanywa kwa kipindi cha miezi nne kutoka Januari ,Aprili, Juni
na Agosti 2021 Dk Abubakar Rajab alisema
kwamba kwa mujibu wa utafiti huo umegundua baadhi ya vyombo vya habari bado
vina uchache wa habari zinazolenga wanasiasa wanawake na uongozi.
Alisema
habari nyingi za wanasiasa wanawake kuwa ni chache na hata hizo chache zimewekwa
katika kurasa za ndani kuazia kurasa ya tano au kurasa za ndani zaidi.
Katika
utafiti huo gazeti la mwananchi limeonekana kwa kiasi limeongeza kutoa taarifa
juu ya wanawake na uongozi wa siasa kulikoni Zanzibar leo ambalo ni gazeti la
serikali Visiwani Zanzibar.
Baada
ya uwasilishwaji wa ripoti hiyo Mhariri Mtendaji Zanzibar leo Ali Haji Mwandini
alionyesha kuguswa na kusema “Utafiti huu utatuwezesha Zanzibar leo kujipanga
upya ili kuongeza kasi ya kutoa habari za jinsia ya kike na uongozi kwa upana
zaidi” .
Kwa
upande wake Muandishi Mkongwe Hawura Shamte alisema ni vyema utafiti mwengine ukaangalia
na uwepo wa picha za wanasiasa wanawake
na uongozi kwani picha huwa zinatoa maelezo mengi kuhusiana na tukio.
“Picha
ni nzuri sana inaweza kuleta mvuto mkubwa kwenye utafiti kwani picha moja
inatoa ujumbe zaid ya maneno 1000 na maneno hayo yanaweza kuleta maana na
tafsiri mbali mbali” alisema Hawura.
Mapema
mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Dk.Mzuri Issa amewataka
waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya jamii ya wanawake na
kuona sauti zao zinasikika kupitia vyombo vya habari.
‘’Vyombo
vya habari vyetu bado vinawajibikakwa kiasi kikubwa kutoa taarifa za jamii ya
wanawake ili sauti zao ziweze kusika hatua ambayo itasaidia kupiga hatua za
maendeleo kwa kuibuwa changamoto zinazowakabili’’amesema.
0 Comments:
Post a Comment