Masauni apiga tafu Jimboni kwake

 


Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Alhaj Hamad Yussuf Masauni amekabidhi Magongo na Gharama za uwezekaji wa Paa katika Chuo cha Madrasatul Ndamba iliyopo Miembeni Wilaya Mjini Unguja

 

Hatua ya kukabidhi vifaa hivyo ni muendelezo wa utekelezaji wa Ahadi zake ikiwa ni sehemu ya Pili ya ziara anazoendelea kuzifanya katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo

 

Akiwa katika ziara hiyo aliyoifanya Jana (Jumatatu 29 Novemba, 2021) aliongozana na Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Kikwajuni Ukiongozwa na Mwenyekiti wa Jimbo hilo Nd Mvita Kibendera pamoja na viongozi wengine wa kamati ya Siasa ya Jimbo

 

Alhaj Masauni amesema atahakikisha anatumia uwezo wake wote kwaajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo huku akitilia mkazo kwenye changamoto za upatikanaji wa Elimu na uwezeshaji wananchi kiuchumi

 

"Heshima muliyonipa Wananachi wa Kikwajuni ni kubwa mno na mimi nafanya yote haya kwasababu ya heshima muliyonipa hivyo nitaendelea kutumia rasilimali zote ili kuhakikisha nakabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kwenye kusaidia utoaji wa Elimu bora na Misingi ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi" alisema Masauni

 

Akikubali ombi la kuwa Mlezi wa Madrasa hiyo Alhaj Masauni amesema ipo haja kwa Uongozi wa Mfuko wa Elimu wa Jimbo hilo kuzipitia madrasa zote zilizopo Jimboni ili kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha zinafikiwa na fursa mbalimbali zitokanazo na Mfuko huo aliyouanzisha kwa lengo la kusaidia harakati za Elimu ndani ya Jimbo

 

Aliwataka Uongozi wa Madrasa hiyo pamoja na wananchi wote kubuni miradi mbalimbali ya Maendeleo itayosaidia kuwaingizia kipato kwaajili ya kuendesha shughuli mbalimbali

 

"Natoa Rai kwa Uongozi wa Madrsa lakini na kwa Wananchi wote wa Jimbo hili, tafuteni miradi yenye tija ambayo yatawasaidia kiuchumi na mie nitakua tayari kuwawezesha ili kufanikisha malengo hayo" alisema Masauni

 

Mapema Mwalimu Mkuu wa Madrasa Damba Sheikh Mohammed Othman amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwafikia na kuteleza ahadi hiyo hali itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza kwa ujenzi huo na kutatua changamoto ya uhaba wa eneo la kuwafundishia watoto wa madrasa hiyo

 

Alifafanunua kuwa ipo haja kwa wazazi kutoa Mashirikiano ya kutosha ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada ili kusaidia uendeshaji wa Madrasa hiyo ikiwemo mishahara ya walimu

 

Katika Hatua nyengine Mhandisi Masauni aliendelea na ziara katika eneo la Mpirani kuzungumza na Wananchi wa eneo hilo na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili

 

Alimalizia ziara yake kwa kuwatembelea Wazee akiwemo Bi Attiy Salim Said katika makaazi yake yaliyopo Miembeni Mjini Unguja

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment