| Mkuu wa Wilaya ya magharibi B Unguja Suzan Kunambi akizungumza na wavuvi katika Diko la Mtoni Kigomeni |
Mkuu wa Wilaya ya
Magharibi A Bi. Suzan Peter Kunambi ameshauri Wavuvi kujiunga katika vikundi
ili kufanya kazi zao kwa mashirikiano lakini pia iwe rahisi kupata fursa
zinazotolewa na Serikali ikiwemo mikopo.
Ameyasema hayo
huko Katika diko la Mtoni Kigomeni alipokuwa akizungumza na Wavuvi wa eneo hilo ,kwa lengo la kuwahamasisha
kuanzisha vikundi vya ushirika.
Amesema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa program maalum ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
na wavuvu ni moja kati ya kundi yatakaonufaika na mpango huo hivyo ni vema kuwa
tayari kwa kufuata mashariti kwani watakaonufaika na fursa hiyo ni wale watakao
kuwa wamesajiliwa rasmi .
Amefahamisha kuwa
mikopo hiyo haitakuwa na riba masharti magumu itatolewa kupitia fedha za IMF
Uviko 19.
Mkuu huyo wa Wilaya
amezitaja fursa zinazotarajiwa kutolewa na Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa
bluu ni pamoja na kuwapatia wavuvi boti
zenye mashine na zana zote za uvuvi na mafunzo maalum ya teknologia bora ya
uvuvi.
Dhamira ya Serikali ni kuleta mageuzi makubwa
katika shughuli zote zinazofanywa na Wavuvi wa maji madogo lakini pia katika
eneo la bahari kuu ili kupata maendeleo
ya haraka na kuimarisha Uchumi wa bluu nchini .
Amewasisitiza kwa wale
watakaobahatika kupata mikopo hiyo kuitumia vizuri na kuirudisha kwa wakati ili
na wengine wanufaike.
Wakitoa changamoto zao
kwa pamoja Wavuvi hao wamesema,Miundombinu ya Mabanda wanayotumia kwa sasa
hayaridhishi pamoja na kukosekana kwa huduma ya Maji safi na Salama na huduma
ya vyoo katika Eneo hilo imekuwa ni changamoto inayowapelekea usumbufu katika
Shughuli zao.
Aidha wameiomba
Serikali kuwapatia ufumbuzi kwa haraka kwa vile maji na huduma ya choo ni
muhimu katika mikusanyiko ya watu.
Aidha wametoa shukurani zao kwa Mkuu huyo
wa Wilaya kwa kufika katika eneo
hilo kuwaelimisha na kuwaeleza dhamira njema ya Serikali kwao.
Wamesema wamefurahishwa na ujio wa Mkuu huyo
katika eneo lao kwani amejionea
mwenyewe Mazingira magumu na hali halisi wanayopitia wavuvi hao .
Wamesema Imani yao kwa Serikali ya Wilaya ni watapatiwa ufumbuzi kwa haraka wa
changamoto zao
Akijibu kuhusu
changamoto zilizotolewa na wavuvu hao Mkuu huyo amewataka Wavuvi hao kuwa na
subra katika kipindi hichi,kwani
Serikali kupitia Manispaa ya
Magharibi A Ina mpango wa kuboresha eneo hilo kwa kujenga Mabanda ya uhakika na ya kisasa ili kuwafanya wavuvi hao wafanye
shughuli zao katika mzingira mazuri.
0 Comments:
Post a Comment