Mke wa Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Zainab Kombo Shaib ametoa wito kwa jamii
kuzingatia malezi na maadili mema katika kuwasimamia watoto yatima ili kujenga
msingi bora wa maisha yao ya baadaye.
Mama Zainab ameyasema
hayo leo alipotembelea Ofisi za Jumuiya ya Muzdalifa na kuongoza hafla ya
kuwagawia sadaka watoto yatima, iliyofanyika katika Ukumbi wa Sebleni kwa
Wazee, Jijini hapa.
Amesema licha ya dhima
ya mahitaji, huduma za msingi na matunzo ya huruma wanayohitaji watoto
walioondokewa na wazazi, bali la msingi ni pamoja na kuzingatia malezi bora na
maadili, yatakayopelekea sehemu hiyo muhimu ya jamii kujengeka na kukubalika
katika maisha ya baadaye.
Akitilia mkazo suala
la malezi bora na maadili kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira
magumu wakiwemo wenye mahitaji maalum, Mama Zainab amewaasa wanafamilia
kutokiuka wajibu wa matunzo, kwa kutegemea huduma za vituo vya kulelea yatima
pekee, pindipo inapotokea miongoni mwa wazazi au walezi kufariki dunia.
sambamba na hilo Mama Zainab aliwausia watu ambao wameondokewa na ndugu zao na kuacha watoto ni vyema wakawalea Mayatima yao kwani watajisikia zaidi wakiwa katika familia zao.
"Ametangulia mbele ya Haki kaka kwa nini ndugu au Shangazi asimlee mtoto wa ndugu kwani na yeye mwanae kuliko kumpeleka katika vituo" alihoji Mama Zainab
Alieleza kuwa hasemi ni vibaya kuwapeleka watoto kulelewa kwenye vituo vya kulelea watoto Yatima lakini alishauri kuwa ni bora watoto wakalelewa na familia zao.
Katika hafla hiyo, Mama Zainab alikabidhiwa Ngao maalum ya Utumishi na Kujitolea katika Kusaidia Watoto Yatima, Wenye Ulemavu na Wanaoishi katika Mazingira Magumu, iliyodhaminiwa na Jumuiya ya Muzdalifa.| Mama zainab Kombo Shaib akimkabidhi mtoto Arwa Rajab Omar sada iliyotaayarishwa na jumuiya Muzdalifa katika khafla iliyofanyika Amani kwa Wazee Zanzibar |
Naye Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Muzdalifah, Sheikh Farouk Hamad Khamis ameeleza azma ya taasisi yake
kuungamkono juhudi za kuwahudumia watoto yatima na wale wanaoishi katika
mazingira magumu, wakiwemo wenye mahitaji maalum, ili kusaidia malengo ya
Serikali katika maendeleo na ujenzi wa ustawi bora wa jamii, katika visiwa vya
Unguja, Pemba na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla.
| Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifa Sheikh Farouk Hamad Khamis akizungumza na watoto Yatima na wazee waliohudhuri katika khafla ya mke wa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzuba Hapo kwa Wazee Zanzibar |
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na viongozi na watendaji mbali mbali wa Serikali, asasi za kiraia,
jumuiya za kusaidia watoto yatima, Idara ya Ustawi wa Jamii, na wazazi.
| Baadhi ya wazee wa watoto Yatima walihudhuria katika khafla ya mke wa makamu wa kwanza wa Rais aliyofanyika Aman kwa wazee Zanzibar |
0 Comments:
Post a Comment