Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewapongeza viongozi na wazee wa
Tumbatu kwa hatua nzuri iliofikia ya kukubali kumaliza tofauti zao zilizodumu
kwa muda mrefu.
Hemed ameleza
hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha Viongozi pamoja na wazee wa Tumbatu
kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema serikali ya
awamu ya nane inayoongozwa na Rais. Dk. Mwinyi imedhamiria kuwaletea maendeleo
wanachi wake waliopo katika Kisiwa cha Tumbatu, hivyo kufikia hatua hiyo la kupatikana
kwa suluhu itakwenda kushajihisha serikali kufikia azama yake ya kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi wake.
Makamu wa Pili wa Rais
amewakumbusha viongozi na Wazee wa Timbatu kuendelea kuzitumia hekima na busara
zao kwa ajili ya kuwaongoza vijana kuwa kitu kimoja na kuachana na tabia ya
kubaguana jambo litakalopelekea mapenzi na huruma miongoni mwao.
"Kwa umoja wetu tusibezane, tusichukiane,tusiuziane kwani kuimarisha kwa hayo Tumbatu kwa muda mfupi itapiga hatua za kimaendeleo" Hemed Alisema
Aidha, Makamu wa Pili
wa Rais amewataka viongizi wa Dini kuendelea kukiombea Kisiwa cha Tumbatu na
wakaazi wake kutourudi tena katika maisha ya dhiki na dhulma ili kuondokona na
mateso yaliokuwa yakiwakabili kwa muda mrefu.
Akizungumzia mikakati
ya maendeleo Hemed amewahakikishia wananchi wa Tumbatu kuwa serikali
katika kipindi kisichozidi cha wiki mbili fedha nyingi zitakifikishwa kisiwani
humo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya
Maji, ujenzi wa skuli, vyookwa ajili ya wanafunzi pamoja na kuimarisha sekta ya
Afya.
Katika hatua nyengine
Mhe. Hemed amewaagiza viongozi wa vyama vya siasa kutojiaribu kuingilia
mchakato huo mzuri uliofikiwa kwa kusababisha chokochoko miongoni mwa wanachama
wao wanaowaongoza.
Pia Makamu wa Pili wa
Rais amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kusimamia suala la undwaji wa
Kamati itakayoendelea kuratibu na kuimarisha maendeleo ya suluhu iliofikiwa
kupitia kikao hicho cha Viongozi na Wazee wa Tumbatu.
Nae Muwakilishi wa Jimbo
hilo la Tumbatu Haji Omar Kheir amesema kuna haja kwa wananchi wa Tumbatu
kupiga mstari kwa kuachana na tofauti zao sambamba na kusahau mambo yote mabaya
yaliopita.
Haji Omar Kheir
amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa hatua alioichukua ya kumuagiza Makamu wa Pili
wa Rais kwa kuipatia Ufumbuzi changamoto ya sintofahamu ya wananchi wa Tumbatu
iliodumu kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema kitendo cha
kupatiwa Suluhu kwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kwa wananchi wa kisiwa cha
Tumbatu ni jambo la kihistoria ambapo wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada
hizo za Rais Dk.Mwinyi kwa kuwataka wananchi kuwa kitu kimoja.
Nao, Viongozi pamoja
na wazee waliohudhuria katika kikao hicho wamemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kuwa, kwa niaba ya wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu wamekubali kuzika
tofauti zao zilizopita lengo likiwa ni kushajihisha maendeleo kwa wakaazi na
wananchi wa Kisiwa hicho.
Viongozi hao wameeleza
kwamba, kwa Muda mrefu wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu wameishi katika madhila
na dhiki kutokana na kukosekana kwa umoja, mshikamano na mashirikiano miongoni
mwao hali iliosababisha watu wake kutoshirìkiana kakatika masuala ya msingi
ikiwemo Sherehe na misiba.
Kikao hicho
kimewakutanisha Viongozi wa serikali wa ngazi tofauti, Vyama vya siasa,
viongozi wa Dini, pamoja na wazee wa vijiji vya Tumbatu.
Matukio ya kijamii yanahitajika zaidi kuibua yaliyopo ndani ya jamii. Zanzibar kuna mengi.
ReplyDelete