wafanyabiashara wa Saruji waonywa Pemba

 

Picha na Maktaba





PEMBA

WAFANYABIASHARA ya saruji wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kwa mujibu wa bei elekezi ambayo imewekwa na Serikali ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa maduka ya saruji kwa Wilaya zote za Pemba, Mkurugenzi wa Kumlinda mtumiaji na Umiliki wa bidhaa  bandia  Zanzibar Aaliye Emanuel Juma alisema, wafanyabiashara wamekuwa wakifanya ubadhirifu kwa bidhaa ya saruji licha ya bei Serikali kuweka bei elekezi.

Alisema kuwa, Tume ya Ushindani halala wa Biashara inawataka wafanyabiashara hao kufuata maagizo ya Serikali kwa kuuza bidhaa hiyo kwa mujibu wa bei iliyowekwa kisheria.

Alieleza kuwa, zoezi hilo walilifanya baada ya kuona kwamba baadhi ya wafanyabiasha sio waaminifu, ambapo wamepandisha bei kwa bidhaa hiyo ya saruji mpaka kufikia shilingi 20,000/= jambo ambalo ni kosa.

“Kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 2018 Tume ya ushindani halala wa Biashara imeweka bei elekezi kwa bidhaa hiyo, hivyo ipo haja ya wafanyabiashara kuifuata”, alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa, Serikali imeangalia gharama zote za usafirishaji wa biadhaa hiyo na ndipo ikaweka bei elekezi kwa wafanyabiashara hao, kwani wamekuwa wakiwaumiza wananchi.

“Saruji zinazotoka Tanzania bara ambayo ni samba, dangote na twiga inatakiwa kuuzwa kwa shilingi 16,500 na kwa ile saruji inayotoka Omani inatakiwa kuuzwa kwa shilingi 19,000 kwa upande wa Pemba”, alisema.

Aliwataka wafanyabiashara hao kufika Wizara husika ikiwa kuna tatizo, ili waweze kukaa pamoja na kulitatua kwani wanataka wananchi wapate biadhaa kwa mujibu stahiki kama ilivyoelekeza Serikali na sio kuwakomoa.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa, wakati wa ukaguzi huo waligundua kuwa, hakuna mfanyabiashara yeyote ambae amebandika bei katika bidhaa yake.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha sheria ya tume hiyo, kila mfanyabiashara anatakiwa abandike bei stahikiu kwa kila bidhaa ili kuepusha udanganyifu, kwani wengine huangalia sura ya mtu na ndipo wakatoa bei wanayotaka”, alisema Mkurugenzi.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa bidhaa hiyo walisema kuwa, kuna saruji nyengie wanaweza kuuza kwa bei iliyowekwa na Serikali, ingawa kampuni nyengine hawawezi kutokana na bei kuwa kubwa.

“Saruji ya Tanga simenti hatuwezi kuuza kwa bei iliyowekwa na Serikali, kwani tutapata hasara kubwa, hivyo bora tufunge maduka”, walisema wafanyabiashara hiyo.

Wakala wa saruji ya Tanga simenti Ali Mohamed Juma mkaazi wa Wete alisema, Serikali imeweka bei elekezi kwa bidhaa ya saruji ingawa kwa upande wao haiwezekani kuuza hivyo, kwani watapata hasara kubwa.

“Saruji nyengine zinazotoka Tanzania bara tunaweza kuuza hata chini ya shilingi 16,000 /= lakini kwa hii ya Tanga simenti ambayo tunainua kwa shilingi 15,500/=, hatuwezi kuuza kwa bei iliyowekwa na Serikali kwa sababu gharama zetu hazitorudi”, alisema.

“Mwanzo niliuliza Wizara kuwa nifunge duka ama niache, kwani kwa bei hiyo siwezi kuendelea, waliniruhusu kuuza lakini leo wanakuja kunifungia duka, sijui niwaelewe vipi”, alieleza wakala huyo.

Mfanyabiashara ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, katika bandari ya Wete wamekuwa wakilipa kodi sita, hivyo kwa saruji ya Tanga simenti hawawezi kuuza kwa bei hiyo.

Zoezi la ukaguzi wa bidhaa ya saruji limefanyika baada ya kuonekana wafanyabiashara kuuza kwa bei ya juu hadi kufikia shilingi 20,000/= jambo ambalo sio sahihi, ambapo Tume hiyo imefungia baadhi ya maduka.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment