MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini na Mkoa wa Mjini Kichama akiweka Jiwe la Msingi katika Maskani ya Wazee ya 'Umaskini haukuletwa na CCM' iliyopo Jimbo la Amani Zanzibar. |
MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Mkoa wa Mjini na Mkoa wa Magharibi Kichama Dk.Ali Mohamed SheIn, ameelezea
kuridhishwa kwake na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika Wilaya ya Amani
kichama.
Akizungumza katika mwendelezo wa
ziara yake ya kujitambulisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ndani ya Chama,
huko katika Tawi la CCM Kwa Wazee Unguja, alisema viongozi na wanachama ndani
ya Wilaya ya Amani wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha Chama Kwa kuanzisha
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dk.Shein, ameeleza kwamba maeneo
mbalimbali aliyoyatembelea na kukagua ameona miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotatua changamoto za Wananchi wa maeneo husika.
Alisema miradi inayotekelezwa
ikiwemo ya upatikanaji wa Maji safi na salama, Vikundi vya Ujasiriamali,ujenzi
wa Maskani za Kisasa za CCM na uendelezaji wa Madara ya Itikadi,Mafunzo na
Elimu yote ni miongoni mwa mikakati endelevu ya kuimarisha Chama na wanachama
kujitegemea wenyewe kiuchumi.
Alipongeza Wabunge,Wawakilishi na
Madiwani wanaoshiriki kutekeleza miradi hiyo kwani ni sehemu yao utekelezaji wa
Ahadi walizotoa kwa Wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.
" Nimepewa jukumu na CCM niwe
Mlezi wenu na nimekuja hapa kujitambulisha nimeanza Kwa ngazi za chini kabisa
za matawi na mashina, walipo Wanachama wetu ambao ndio chimbuko na uimara wa
Chama.
Toka nimeanza ziara hii nimeshiriki
shughuli mbalimbali za maendeleo katika Matawi na Mashina, hali inayoonyesha
utekelezaji wa Ilani yetu kwa vitendo,hakika Chama kinaendelea kuwa imara
zaidi.", alisema Dk.Shein.
Alisema Serikali ya Zanzibar Kwa
awamu mbalimbali zimekuwa zikitekeleza miradi ya upatikanaji wa huduma za Maji
safi na salama ili kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Katika maelezo yake Dk.Shein,
aliwasihi wanachama kununua bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya Ujasiriamali
vinavyoanzishwa na wanachama ili mitaji yao ikue na wajitegemee wenyewe.
Akizungumza katika Maskani ya
shukrana iliyopo Jimbo la Chumbuni alisema Maskani zilizozinduliwa zitumike
kufanyakazi za Chama Kwa kuongeza zaidi wanachama wapya.
Alisema viongozi wa CCM waendelee
kufanya kazi za kisiasa Kwa kuwa mfano bora wa kusema na kuonyesha maendeleo
Kwa vitendo ili Wananchi walio nje ya Chama wavutiwe na Sera za CCM na kujiunga
na Chama kwa wingi.
Dk.Shein ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, alisema katika juhudi za kuimarisha Chama ni lazima
wanachama walipe Ada Kwa wakati.
Alisisitiza wanachama kuendelea
kupendana na kuheshimiana kwani Chama hakiwezi kujengwa Kwa kuchukiana.
"waasisi wetu katika harakati
za ukombozi walipenda,kushirikiana na kuchangishana michango mbalimbali Kwa
hiari ndio maana walifanikiwa kufanya Mapinduzi ya Januari 12,mwaka
1964".alisisitiza Dk.Shein.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dk.Juma Abdulla Mabodi, alisema ziara hiyo ni miongoni mwa maelekezo
ya Kamati Kuu ya CCM ya kuhakikisha Viongozi wanashuka kutembelea ngazi
za matawi na mashina kwa lengo la kuimarisha Chama.
" Tunaamini Wana CCM mnafanya
kazi kubwa na iliyotukuka katika maeneo yenu na ndio maana viongozi wenu
wamekuja katika maeneo yenu kukaa nanyi Kwa lengo la kubadilishana mawazo na
kujionea wenyewe changamoto na mafanikio yaliyofikiwa",alisema Dk.Mabodi.
Kwa upande wake Balozi wa Shina
namba 2 katika Tawi la CCM Mpendae Juu Khadija Hassan Salmin, alikishukru Chama
kwa kuisimamia vizuri Serikali iliyotekeleza vizuri mradi wa ujenzi wa mtararo
mkubwa wa kupitisha Maji ya mvua na kutatua kero ya mafuriko kwa Wananchi wa
Jimbo la Mpendae na maeneo jirani.
Aidha alikiomba Chama kuanzisha
utaratibu wa kuwalipa posho Mabalozi wa mashina kwani nao wanafanya kazi kubwa
ya kukijenga Chama, hivyo fedha hizo zitawasaidia katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu
wa Ushirika wa 'Uvivu hauna Maendeleo' Kilichopo Kilimahewa Bondeni,
Mtende Jirani Mtende alisema kikundi kinachotengeneza bidhaa mbalimbali
zikiwemo ususi wa mikeka,mikoba na ushoni wa nguo niwanakabiliwa na changamoto
ya ukosefu wa Soko,ukosefu wa Ofisi ya kudumu,mikopo nafuu na ukosefu wa Elimu
ya Ujasiriamali.
Katika ziara hiyo Dk.Shein
aliyembelea maeneo mbalimbali yakiwemo kupandisha bendera Shina namba mbili
Mpendae Juu,kumtembelea mwasisi wa Chama Ali Omar Ali(Chengo),kuweka jiwe la
msingi Maskani ya Wazee ya 'Umaskini haukuletwa na CCM' ,kuangalia Mradi wa
Pilipili 'Hamasa Chill', ametembelea kikundi Cha 'Uvuvi hauna Tija,ametoa kadi
za uanachama Kwa wanachama na jumuiya.
Nyingine ni uzinduzi wa mradi wa
Maji safi na salama uliopo Shehia ya Kwa Wazee,kuweka jiwe la msingi katika
uwanja wa mpira wa Kivumbi na kuzindua Darasa la Itikadi na kutoa kadi za CCM
Kwa wanachama wapya Jimbo la Shauri Moyo
0 Comments:
Post a Comment