Waziri Rahma akerwa na kuzorota ujenzi wa bandari

 

Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Rahma Kasim Ali

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali ameunda timu ambayo itaweza kufuatilia kwa karibu ujenzi wa bandari ya mkokokotoni kwa kile kilichonekana kuwa bandari hiyo imekua imechukua muda mrefu katika utekelezaji wake  kinyume na makubaliano ya awali wa mkataba wao baina ya serikali na mkandarasi.

 

Akizungumza katika ziara ya kukagua ujenzi huo uliopangwa kukamilika mwezi huu wa septemba amesema hajaridhishwa na hatua iliyofikiwa jambo linalochelewesha matumizi ya bandari hiyo hasa katika fursa za kibiashara

 

Amesema uwepo wa timu hiyo utafuatilia kwa karibu zaidi ujenzi ikiwemo kuangalia ubora wa ujenzi ili kudumu kwa muda mrefu kwani imekuwa jambo la kawaida kwa wasimamizi wa ujenzi kujenga kwa kutojali ubora kutokana na sababu za kuharakishwa.

 

Akizungumzia umuhimu wa bandari hiyo waziri Rahma amesema itaweza kusaidia usalama wa wanaovuka kwenda kisiwa cha tumbatu pamoja na kupunguza urefu wa masafa ya wanaosafiri kwenda pemba,tanga na bagamoyo

 

Nae mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amehimiza watendaji wa bandari kuanza matayarisho ya ujenzi wa majengo yaliyo ncje ya mradi huo yakiwemo maeneo ya kuhudumia watakaotumia bandari hiyo ikiwemo ofisi za kuuzia tiketi  sehemu za huduma za kijamii pamojab na vituo vya afya ili ujenzi utakapokamilika kuanza kazi moja kwa moja.

 

Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo alimkumbusha wajibu wake msimamizi wa mradi huo ambao ni wakala wa majenzi Zanzibar  kusimamia vyema kwa kuhakikisha anapita mara kwa mara ili kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati na kwa kiwango kilichopangwa.

 

Aidha mhe ayoub amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha muda wa miezi mitatu aliomba kutoka serikali ahakikishe anajipanga vyema ikiwa ni kuongeza kwa vifaa na wafanyakazi ili aweze kwenda sambamba na muda aliomba.

 

Kwa upande wa wananchi Ayoub aliwatoa hofu wananchi wa mkoa huo kwamba serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha mradi huo unamaliza kwa wakati na ifikapo januari bandari hiyo itaanza kutumika

 

 

 

 

Akitaja sababu za kuchelewa kukamilika kwa mradi huo injinia Ediel kimaro kutoka kampuni ya Edge consultation .amesema  imetokana upatikanaji wa mawe ulikua wa shida jambo ambalo liliwafanya wakae miezi 2 bila ya kufanya kazi.

 

Aidha Mkandarasi huyo aliahidi kumaliza kazi hiyo kwa muda aliomba na kwa sasa kazi hiyo imefika asilimia 75 ambapo alisema hivi sasa wanamalizia kazi ya ujazaji mawe na hivi punde wataanza kazi ya uwekaji zege 

 

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment