Makamu wa kwanza ataka waalimu wajengwe uwezo ili wende sambamba na kasi ya mabadiliko ya Dunia

 

Makamu wa kwanza Othman Masoud Othman akifungua Kongamano la walimu katika ukumbi wa Idrisa Abdul wakili Kikwajuni  Zanzibar 



MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar,  Othman Masoud Othman, amesema kwamba ni muhimu kwa walimu kujengewa uwezo zaidi ili kuwa sambamba na mahitaji ya elimu yanayokwenda na kasi ya mabadiliko ya dunia.

Makamu ameyasema hayo leo, alipofungua kongamano la walimu huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni mjini Zanzibar, ikiwa ni matayarisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Walimu Duniani inayoadhimishwa tarehe 5 Oktoba, ya kila mwaka.

 Amefahamisha kwamba, hivi sasa elimu imetanuka sana kutokana na kuwepo kasi kubwa ya mabadiliko na maendeleo ya sayansi na Teknolojia na kwamba katika mazingira hayo ni vyema kuwepo mikakati madhubuti itakayosaidia  kujenga mfumo bora na imara wa  kuwaongeza uwezo wa walimu hapa nchini.

Akizungumzia hadhi ya  walimu hapa Zanzibar, Othman amesema  imeshuka na kuitaka jamii na hasa walimu  kuweka mikakati ya suluhisho la vikwazo katika maendeleo ya elimu .

Kuhusu maslahi ya walimu, Mhe. Othman amesema serikali inaendelea na juhudi za kuleta mageuzi ya elimu na suala hilo linasubiri idhini ya serikali ili hatua zaidi kuchukuliwa.

Aidha kuhusu mapambano dhidi ya unyanyasaji wa watoto, amewataka walimu kushirikiana na Polisi, Wanasheria na Mawakili kuandaa mkakati shirikishi utakaongoza na kusimamia vyema mapambano dhidi ya  tatizo hilo.

Kuhusu haki za walimu  Makamu ameshauri kutumia utaratibu  wa majadiliano  baina ya walimu na serikali ambayo ni kazi isiyo na gharama kwa kusaidia kujenga mfumo utakachangia kuondosha matatizo  yao.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Simai Mohammed Said, amesema serikali kupitia wizara hiyo inakaribisha kuwepo majadiliano na waalimu ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

 

Katika risala yao iliyosomwa na Mwalimu Haji Juma Omar, wameipongeza Serikali kutokana na juhudi kubwa za kutia moyo zinazofanywa katika maendeleo ya sekta ya elimu pamoja na kuendeleza maridhiano ya serikali ya Umoja wa kitaifa

Hata hivyo, wametanabahisha serikali kufahamu kwamba, skuli nyingi zinakabiliwa na changamoto za kimazingira ikiwa ni pamoja na kukosekana hati miliki na kusababisha maeneo mengi kuvamiwa kwa shughuli za ujenzi wa makaazi.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment