Mwandishi wetu, Arusha
Shirika la Kimataifa la
watetezi wa haki za Binaadamu la DefendDefenders na Taasisi ya wanahabari ya
kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) wamewataka wanahabari kufanya kazi kwa
weledi huku wakijali afya zao.
Akizungumza katika
ufunguzi wa mafunzo ya siku Tano ya wanahabari jijini Arusha, Kuhusiana afya
,kuondoa msongo wa mawazo na Uandishi Bora wa habari za Uviko-19, Afisa Kitengo
ya Ulinzi na Ustawi wa shirika la DefendDefenders East and Horn of Africa, Karis
Moses alisema wanahabari ni kazi nzuri na inachangamoto nyingi.
Moses alisema kazi za
Uandishi wa habari na utangazaji zinakawaida kuwa changamoto ambazo husababisha
msongo wa mawazo na bila kupata tiba
unasababisha Maradhi hivyo ni muhimu sana kujali afya zao.
"Kazi zenu ni
ngumu na mnapaswa kuwa na utaratibu za kukabiliana na changamoto za
kisaikolojia ambazo kama hazifanyiwi kazi huwezi kusababisha Maradhi ambayo
yataathiri utendaji kazi wetu "alisema
Muuguzi Sam Sangalo
alisema ni muhimu wanahabari kutenga muda wa kupumzika ,kufanya mazoezi,kupata
lishe bora na kujiepusha na mambo ambayo yatawapa msongo wa mawazo wenye athari
kwao.
Mjumbe wa bodi ya
shirika la watetezi wa haki za Binaadamu Tanzania(THRDC) Edwin Soko akifungua
mafunzo hayo aliwataka wanahabari kufanya kazi Kwa weledi ili kazi Yao iwe na
tija katika jamii.
Soko alisema jamii kwa
kawaida ina imani kubwa na wanahabari
wanaojitambua kama ndio watetezi wao kutokana na kupaza sauti zao na
kuibua changamoto zao ili serikali na Wadau wengine wazifanyie kazi.
Mkurugenzi wa Taasisi
ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) Mussa Juma alisema lengo
la mafunzo hayo ni kuwakumbusha wanahabari wajibu wao katika jamii lakini pia
kujali afya zao.
Juma alisema wanahabari
wakijua wajibu wao katika jamii watasaidia kupunguza changamoto ikiwepo
upotoshwaji juu ya ugonjwa wa uviko-19 na Chanjo na hivyo Wananchi wengi
kujitokeza kupata chanjo.
Waandishi wa habari 20
Kutoka mikoa Saba wanashiriki mafunzo hayo ambayo yatakwenda sambamba na kupata
chanjo ya Uviko-19 , kutembelea hifadhi ya Taifa kujifunza na kujifunza
uchoraji kama njia pia kupunguza msongo wa mawazo.
0 Comments:
Post a Comment