Na Fatma Sleiman,Pemba
fsleiman@marhabanews.net
Wazazi na walezi kisiwani Pemba wametakiwa kuekeza kuwalea watoto wao katika misingi bora ya kiimani ya dini ya kiislam itakayowasaidia hapa duniani na kesho Akhera.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Leila Mohd Mussa katika Maazimisho ya mahafali ya kituo cha Marhemed cha nasar school kilichopo ole kisanga ambacho pia kinafundisha na elimu ta Tahfidhl Quran kwa watoto.
Amesema Kutokana na dunia kuzungukwa na mambo ya utandawazi ni vyema wazazi kuwapeleka watoto wao katika vituo ambavyo vinafundisha masuala mbali mbali yakiwemo ya imani za kiislam ili kuwajenga watoto wao katika misingi bora.
Aidha Wazir Leila amewafahamisha wazazi kulipia ada ambazo zitawasaidia walimu kuendelea kuwafundisha watoto wao bila kikwazo chochote.
Akisoma Risala katika hafla hiyo Maalim Seif Khamis Nassor ameeleza miongoni mwa changamoto zinazorejesha nyuma maendeleo yao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa kulipia ada kwa wazazi .
Kituo hicho cha Marhemed kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanafunzi 77 na wealimu 4 ambapo kwa sasa kimefikia wanafunzi 193 na walimu 13 wakiwemo walimu wa atahfidhl kuran na walimu 7 wa kusomesha Nassar na Primary.
0 Comments:
Post a Comment