NA IS-HAKA
OMAR,ZANZIBAR.
SERIKALI ya Mapinduzi
Zanzibar imesema inaendelea na juhudi za kuwahamasisha wananchi waendelee
kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Kauli hiyo ameitoa
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Leila Mohamed Mussa, mara baada ya
kushiriki ziara ya kutembelea vivutio vya utalii katika maeneo ya Fukuchani na
Mvuleni uko Mkoa wa Kaskazini Unguja ya Wajumbe wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT) kutoka Pemba.
Alisema utalii ni
sekta muhimu inayoingizia Serikali fedha nyingi za kigeni zinazochangia kukuza
uchumi wan chi.
Leila alieleza kuwa
serikali imeendelea kuweka mikakati imara ya kuhakikisha wananchi wazawa nao
wanakuwa ni sehemu muhimu ya wadau wa utalii kwa kuhakikisha wanatembelea
vivutio vya utalii na kuchangia fedha zinazoongeza kukua kwa pato la taifa.
Akizungumzia ziara
hiyo Waziri huyo Leila, alisema UWT wameamua kutembelea vivutio hivyo ikiwa ni
hatua ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa ni kinara wa
kutangaza sekta ya utalii kitaifa,kikanda na kimataifa.
Katika maelezo yake
Waziri huyo aliwasihi wananchi mbalimbali wanaoishi katika maeneo yenye vivutio
vya utalii kuhakikisha wanalinda rasilimali hiyo ili kuzuia uharibifu wa maeneo
hayo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
“Natoa wito kwa
wananchi waendelee kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vyetu vya utalii ili
kujifunza na kujua mambo mengi kuhusu utalii na nchi kwa ujumla.
Leo nimeungana na
wajumbe wenzangu kutoka Pemba tumetembele maeneo mbalimbali ya vivutio vya
utalii tumepata historia ya maeneo hayo ambayo imetuongezea uelewa mkubwa
katika shughuli zetu za kisiasa.”, alisema Waziri Leila.
Naye Mwenyekiti wa UWT
Mkoa wa Kusini Pemba Bimkubwa Khamis Mohamed, alisema ziara hiyo imekuwa na
manufaa kwa kuona na vivutio vyenye historia nzuri ambayo awali hawakuijua.
Alisema kupitia ziara
hiyo imemjenga kuwa balozi mzuri wa kutangaza utalii wa ndani hasa kwa wanawake
na vijana ambao wengi wao wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya utalii.
Bimkubwa, alipongeza
Waziri huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa
kuratibu ziara hiyo iliyowaongezea uelewa juu ya masuala ya utalii.
Kwa upande wake Sheha
wa shehia ya Fukuchani haji Mohamed Juma, alisema serikali imevumbua maeneo ya
Kale katika shehia hiyo ambayo yalikuwa wakiishi watu katika karne ya 15 na 16
jambo ambalo ni faraja kwa wakaazi wa eneo hilo.
Haji, alizija fursa
mbalimbali wanazonufaika wananchi zikiwemo vijana kujiajiri na kupata kipato
kinachotokana na kutembeza watalii wanaofika katika maeneo hayo.
Maeneo
yaliyotembelewa ni eneo la Fukuchani yenye majengo ya kihistoria lililokaliwa
na Wareno,kaburi la mtu mrefu aliyejulikana kama Bi.Banji Faraji pamoja na
pango la Ajabu katika eneo la Mvuleni.
0 Comments:
Post a Comment