Wakati utekelezaji wa mradi wa Viungo visiwani Zanzibar ukingia mwaka wa pili kamati ya ushauri
ya mradi huo (ZIMAG) imefanya ziara ya kukagua baadhi ya mashamba ambayo ni ya
wanufaika wa mradi huo katika maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Unguja.
Ziara ya ukaguzi huo wa mashamba iliongozowa na
Mwenyekiti wa kamati hio Mohamed Khamis Rashid pamoja na wajumbe wengine ambao
ni wa kamati hio pamoja na Meneja mkuu wa
utekelezaji mradi Amina Ussi Khamis.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara Mwenyekiti wa
kamati hio ambae pia ni Mkurugenzi idara ya kilimo Zanzibar alisema wamejifunza
mengi kupitia ziara hio ikiwemo kuona maendeleo makubwa ya wakulima ambao ni
wanufaika wa mradi wa Viungo.
Alisema cha kufurahisiwa zaidi kuona mradi huo
umejikita kwa walengwa na kwa kiasi
kikubwa kuna maendeleo ambayo yameifariji kamati hio ya ushauri.
Alieleza kuwa wao kama wajumbe wa kamati imewanufaisha kwa kiasi kikubwa ikiwemo kujua
kinachoendelea na wataendelea kufanya ziara nyengine zaidi kila muda.
Sambamba na hayo aliwataka wakulima katika maeneo
mbali mbali ya Unguja na Pemba kuitumia fursa ya mradi huo kama sehemu ya
kujiendelea kiuchumi na wasikubali kabisa kutojihusha na mradi huo kwa kuwa ni
aina ya mradi ambao una malengwa makubwa ya kuwainua wananchi kiuchumi.
‘’Ninapenda kutoa wito kwa wakulima wote katika
kipindi hichi cha utekelezaji wa mwaka wa pili wa mradi huu kuhakikisha
wanajitokeza kwa wingi kujisajili ili wanufaika wengi zaidi waweze kupatikana’’aliongezea.
Awali Meneja utekelezaji mradi huo Amina Ussi Khamis
alisema ziara ya wajumbe hao imeratibiwa kwa lengo la kukusanya maoni ya kamati
hio ya ushauri ili waweze kutoa ushauri baada ya kuona kile kinachoendelea
shambani.
Alieleza kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja mradi huo
umeshafanya mengi ambayo wajumbe wakamati hio ya ushauri wangepeswa kuyaona na
na kuja na ushauri utakao jenga zaidi na kuleta tija.
Mmoja miongoni mwa wakulima ambae anajihusisha na
uzalishaji wa miche ya miti ya Matunda Kurwa Othman Chande alisema kupitia
mradi ameongeza elimu na ujuzi ambao awali hakuwahi kuwa nao na ndio kitu pekee
hivi sasa anachoendelea kujivunia.
Alisema kupitia mradi wa viungo umefanya kuongeza ari
zaidi ya uzalishaji wa miti tofauti ya matunda na kuwauzia watu mbali mbali
jambo ambalo anaamini limekuza soko lake.
Mkulima mwengine wa pilipili boga kutoka shehia ya mwache alale Sheikha Khamis Sheikha alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huo walikua wakifanya kilimo hicho lakini hakikua na manufaa makubwa.
Alisema mara baada ya kutekeleza mradi huo hivi sasa wanafika hadi kuvuna pilipili boga kilo 2000 na wametanua soko zaidi kwa kuuza bidhaa hizo Bagamoyo.
Alisema uamuzi wa kuuza bidhaa hizo nje ya Zanzibar
umetokana na changamoto kubwa ya masoko visiwani hapa pamoja na ulanguzi
aliodai unafanywa na madalali katika masoko mbali mbali.
Mradi wa huu wa Viungo unatekelezwa katika shehia 60 Unguja na Pemba kwa mashirikiano kupitia taasisi ya PDF,CFP pamoja na TAMWA-ZNZ chini ya ufadhili wa umoja wa Ulaya (EU)
0 Comments:
Post a Comment