Mwanasheria Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Omar Said Shaaban apokea wanachama wapya 250




Zaidi ya wanachama wapya 250  wamejiunga na chama cha ACT Wazalendo  na kupokewa na Mwanasheria mkuu wa cha hicho Omar Said Shabaan.

Shaaban aliwapokea wanachama hao huko Kwa Maharouk Jang’ombe Jimbo la mpendae katika shuhuli iliotayarishwa na Ngome ya wanawake ya chama hicho.

Akizungumza katik shuhuli hiyo Shaabani aliwapongeza viongozi wa ngome hiyo kutokana na kazi kubwa wanaiyoifanya ambayo matunda yake yanaonekana.

Alisema kazi ya kuwapata wanachama 250 wakajiunga na chama hicho ni kazi ngumu na ya kupigiwa mfano, na kutokana na kazi hiyo aliwapatia zawadi ya laki tatu  kwa juhudi zao.

Sambamba na hilo Shaaban aliwaambia wanachama hao kujisikia kama wao wamejiunga na chama hicho muda mrefu kwani wana haki sawa na wengine

Mapema Mwenyekiti timu Mkakati ya Ngome hiyo Pavu Abdallah allisema wanachama hao walikuwa nao katika chama cha CUF lakini walipohama wao waliobakia huko.

“Lakini leo wameamua kujiunga katika Juhudi za kupigania uwepo wa Zanzibar yenye mamlaka kamili na tunawaambia karibuni tuendeleze mapambano” alisema Pavu.









 



About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment