MCHEZAJI Othman Miraji
ameibuka na ubingwa wa michuano ya Judo ya watoto yaliyofanyika katika ukumbi
wa Chama Cha Judo uliopo Amaan mjini Unguja.
Mashindano hayo ya
siku mbili yaliandaliwa na chama cha mchezo huo na kushirikisha watoto kuanzia
mika sita hadi 14.
Katika mashindano hayo
bingwa alikabidhiwa medali ya dhahabu, cheti cha ushiriki na baskeli, wakati
nafasi ya pili iliyokwenda Haris Mohamed alipata medali ya fedha, cheti na rice
cooker.
Zawadi ya mshindi wa
tatu ambayo ni medali ya shaba, cheti na Electric kettle, ilichukuliwa na
washiriki watatu ambao ni Lukman Abdulla, Mbarouk Farouk na Abdillah Mgeni.
Mashindano hayo
yaliyofanyika Novemba 28 mwaka huu, yalishirikisha wachezaji 53 kutoka maeneo
mbali mbali mbali ya ya Zanzibar, ambapo na kupatiwa zawadi washindi lakini
washiriki wote walipatiwa fulana.
0 Comments:
Post a Comment