MAKAMU Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, amesema
ni muhimu kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) kuongeza ubunifu
katika utoaji wa huduma kuwa na kiwango cha kimataifa na zinazohimili
ushindani wa biashara ya Fedha dunaini.
Othman ameyasema hayo leo Ofisini kwake Mingombani mjini
Zanzibar alipokutana na Uongozi wa Benki ya PBZ, uliofika ofisini kwa makamu
kujitambulisha na kushauriana naye juu masuala mbali mbali kuhusu Benki hiyo.
Amesema hivi sasa Zanzibar kuna Benki nyingi zinazofanya kazi ya
utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi na wageni jambo ambalo linaongeza
ushindaji kwa kuwa wateja wengi wanaojiunga na huduma za benki zinazoanzishwa
pia ndio wanaohitajika na PBZ.
Aidha Makamu amesema kwamba pamoja na jitihada kubwa
zinazofanywa na uongozi wa Benki hiyo kuimarisha hudma, lakini bado zipo
changamoto mbali mbali zikiwemo za urejeshaji wa mikopo kutoka kwa wateja wake
pamoja na kuwepo mifumo ya kisheria ndani ya benki hiyo inayohitaji
kufanyiwa marekebisho ili kwanda na wakati wa ushindani wa biashara
hiyo.
Alishauri Uongozi wa PBZ kufanya marekebisho katika baadhi
ya sheria ili kuimarisha taratibu zinazosimamia benki hiyo kwa nia ya kuweka
mfumou bora zaidi wa utoaji wa huduma na kusaidia kuwavuta zaidi wateja
wake kuendelea kuitumia Benki hiyo .
Aidha aliutaka Uongozi wa Benk hiyo kuendelea kuitumia fursa ya
Uzalendo wa Wananchi na Wafannyabiashara wa Zanzibar kuendelea kuipenda Benki
yao kwa kupata huduma bora za Kibenki zitakazowaridhisha ili waendelee kuiamini
kwamba ni benki bora kuliko zote zilizopo Zanzibar.
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Dk.
Muhsin Suleiman Masoud, amesema kwamba pamoja na changamoto mbali mbali
zilizopo katika Benki hiyo, lakini wamekuwa wakijitahidi kuimarisha utoaji wa
huduma bora ili kwenda na wakati na kuhimili ushindani.
Alikiri kwamba urejeshaji wa mikopo kutoka kwa baadhi ya wateja
wake bado inaendelea kuwa changamoto kubwa ambapo hali hiyo inapotokea
mara nyengine huchangia gharama za mikopo kuwa kubwa kwa wateja wa aina hiyo.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema kwamba licha ya Benki hiyo
kupitia katika kipindi kigumu, lakini bado ipo vizuri na inaendelea kuimarika
na wateja wengi wanapenda kutumia huduma za Benki hiyo.
Amefahamisha kwamba hivi karibuni Benki hiyo itaendelea kufungua
matawi mapya katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na
kuongeza mawakala hadi 800 kutoka 200 walipo sasa.
0 Comments:
Post a Comment