Meneja Mahusiano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray.
NA BETTY KANGONGA
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema upo tayari kuwahudumia watanzania mara baada ya Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utakapopitishwa rasmin bungeni.
Hivi karibuni Serikali ilisema kuwa itaanza kutekeleza Mpango wa
Bima ya Afya kwa wote kwa kutenga Sh.Bilioni 149 katika mwaka wa Fedha 2021/22
Mziray alisema, Serikali imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya ili
kuboresha miundombunu ya kutoa huduma ya afya hivyo ni vema watanzania
wakaendelea kujiunga na bima ya afya kwa kuwa gharama zimepunguzwa na zipo
katika makundi mbalimbali.
Amesema NHIF imejiandaa kuhakikisha inaweka mfumo wa Tehama
ambapo watanzania wataweza kujisajili popote walipo kutokana na urahisi
utakaokuwa umewekwa.
Kuhusu maonesho hayo Meneja Uhusuano huyo amesema katika kipindi
cha siku saba katika maonesho hayo watatoa huduma mbalimbali ikiwemo ya usajili
kwa watu wanaotaka kujiunga na Mfuko huo.
Aidha amesema watatumia muda huo kutoa elimu wa wakazi wa Jiji
la Dar es salaam kujua umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya badala ya kusubiri
kuugua ndipo wakate.
0 Comments:
Post a Comment