Kamati ya bajeti ya baraza la wawakilishi Zanzibar imeitaka ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Pemba pamoja na idara zake kuhakikisha wanaendelea kusimamia maradi wa uimarishaji wa msingi wa maji taka katika mji ili uweze kukamilika kwa wakati .
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hio Ali Suleiman Ameir mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa uimarishwaji mfumo wa maji taka huko katika eneo la Msingini na Kichungwani katika mji wa chake chake mkoa wa kusini pemba.
Alisema endapo ofisi hiyo pamoja na idara zake utasimamia mradi huo matokeo chanya yatapatikana baada ya kukamilika mradi huo .
"Ombi langu kwa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais na idara zake lakini pia idara za mazingira na usimamizi wa mazingira ikiwemo zema kuendelea kusimamia mradi huu ili matokeo chanaya mwisho wa mradi huu yaweze kukamilika" alisema .
Hata hivyo mwenye kiti huyo aliwataka wananchi ambao watatumia moja kwa moja mradi huo kuupokea mradi huo na kuutumia kwa uanagalifu ikiwemo kuitunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Omar Dadi Shaka alisema kuwa bado wananchi wamekuwa na uelewa mdogo juu ya atahari za mabadiliko ya tabia ya nchi jambo ambalo hupelekea kurudisha nyuma juhudi zinazofanywa na serikali katika kuimarisha mazingira siku hadi siku
Ipo haja ya kutanua wigo wa kushughulikia masuala ya mazingira ili kuleta maendeleo na kuimarisha miji kiasili katika kutunza na kuhifadhi mazingiara na kupunguza hali ya joto na mabadilko ya tabia nchi katika makazi ya watu.
Ziara hiyo ya kukagua mradi huo wa majitaka ilianzia katika shehia msingini Afrikana na kumalizia banda taka kichungwani .
0 Comments:
Post a Comment