Waziri Mkuya ateuwa wajumbe wapya wa baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Zanzabar

 

Waziri wa Nchi wa Afisi ya Makamu wa kwanza  Rais Zanzibar Sada Mkuya Salum. 



Raya Hamad – 0MKR

 

Waziri wanchiOfisiwaMakamuwa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum amefanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kwa kipindi cha miaka mitatu 2021 – 2023.

 

“Kwa mujibu wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu (Haki na Fursa) Namba 9 ya Mwaka 2006, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamuwa Kwanza wa Rais amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Baraza la Taifa la WatuWenyeUlemavu”

 

Aliowateua ni Mohammed Abdallah Mohammed – kutoka Jumuiya ya Watu wenye Ualbino Zanzibar (JMZ), Nassor Suleiman Nassor kutoka Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ).

 

Kwa upande mwengine waziri Mkuya aliwateuwa  Afwa Nassor Hassan – kutoka Chama Cha Viziwi Zanzibar (CHAVIZA) sambamba na Fatma Djaa Chesa – kutoka Jumuiya ya Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB).


Pia Waziri huyo alifanya utuzi kwa HidayaMjaka Ali – kutoka Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Pamoja na HaroubSoudMzee – kutokaKituo cha Watu wenye Ulemavu na Maendeleo Jumuishi Zanzibar (ZACEDID).


Kwa upande jumuiya ya waajiri na chama cha wafanyakazi Zanzibar pia aliwateuwa  Mohamed Najim Omar – kutokaJumuiya cha Waajiri Zanzibar (ZANEMA), na Sharifa Mohamed Salum – kutoka Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC).

 

Uteuzi huu ni kufuatia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kumteuwa Salma Saadati Haji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu tarehe18 Agosti, 2021.

Uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu, unaanza tarehe 01 Oktoba, 2021.

 

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment