| Hemed akizungumza na wazee pamoja na wananchi waliohudhuria katika kilele cha maadhimisho siku ya wazee duniani kilichofanyika katika viwanja vya skuli ya Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja. |
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ameitaka jamii kutokwepa jukumu la
kuwalea wazee katika kuwapatia matunzo na huduma za msingi.
Hemed ametoa wito
huo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani kilichofanyika
katika Uwanja wa Skuli ya Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema wazee
wanahitaji mapenzi na huruma kutoka kwa Watoto wao na jamii inayowazunguka
hivyo kuna haja kwa familia na jamii kwa ujumla kuhakikisha wazee wanapata
mapenzi hayo wakiwa katika familia zao.
Alieleza kuwa, kuwalea
wazee ndani ya nyumba ni jambo linaloleta barka na fanaka sambamba na kutoa
mafunzo mema kwa Watoto katika kuwalea wazee wao.
“Tufahamu kwamba
vitabu vitakatifu vinaeleza umuhimu na baraka ya kuwatunza wazee, Na tufahamu
kuwa ukimtendea maovu mzee wako Mwenyezi Mungu anakuja kukulipa maovu na wewe”
Alieleza Hemed
Makamu wa Pili wa Rais
aliesema katika kuunga mkono suala hilo Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa
na Rais Dk. Mwinyi imeendelza dhamira na shabaha ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kuweka mikakati ya kuwaendeleza wazee ambayo inaendelea kuimarishwa na kwa
kuendelea kuwatunza wazee wasiokuwa na jamaa wala rasilimali katika makazi
maalum ikiwemo Sebleni, Welezo na Limbani.
Hemed Alifafanua
Serikali imeendeleza matunda hayo kwa kuweka sera na mipnago mbali mbali za
kuimarisha Ustawi na maendeleo ya wazee nchini ikiwemo kufanya mapitio ya
muongozo wa pensheni jamii na kutengeneza kanuni na sheria ya wazee
iliyozinduiwa mwaka 2020.
Alieleza, Mpango wa
Penchini jamii umeweza kuwasiadia kiuchumi baadhi ya wazee walio wengi kwa
kuzitumia fedha hizo katika shughuli ndogo ndogo za uzalishaji mali na
kujiongezea kipato.
Alisema wazee waliopo
katika vituo hivyo Serikali inaendelea kuwapatia huduma zote za msingi
wanazostahiki ikiwemo kuwasimamia, chakula, malazi ,mavazi matibabu pamoja na
posho.
Hemed alisema
Serikali inatambua umuhimu na mchango mkubwa uliotolewa na wazee katika
maendeleo ya nchi na kupelekea kuanzisha program maalum ya kuwapatia pensheni
wazee wote waliofikia uimri wa miaka 70 na kuendelea ikiwa ni utekelezaji wa
sera na hifadhi ya jamii.
Alieleza kwamba, Idara
yenye dhamana na wazee imehakikisha inaendelea kuwasajili wazee wote waliofikia
umri wa miaka sabiini na wananufaika na pensheni hiyo,ili iendelee kuwasaidia
katika shughuli zao za kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea
kuimarisha huduma za wazee ikiwemo afya na usafiri , na kueleza kuwa kwa hatua
ya awali jumla ya wazee Elfu mbili mia nne na arubaini na nane (2,448)
wameshapatiwa vitambulisho maalum vya kuwasaidia kupata huduma hizo kwa
urahisi.
Akigusia suala la
malezi Hemed aliwataka wazee kuendelea kulinda mila, silka na desturi ya
wazanzibar katika malezi, ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji katika jamii
zetu.
Pia Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar akiwa mwenyekiti mwenza wa Kamati ya sensa ya watu na makaazi
Taifa aliwaomba wazee hao kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa kupitia sensa
inayotarajiwa kuanza Mwezi Agosti Mwaka Kesho.
Akisoma risala kwa
niaba ya wazee Maulid Nafasi Juma alisema wazee wa Zanzibar wanampongeza Rais
Dk. Mwinyi kwa kuendeleza Jitihaza zilizoanzishwa na Serikali ya awamu na
sab ana kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika kupambana na vitendo
viovu ikiwemo kupiga vita suala la ubadhilifu wa mali za umma.
Alisema Pamoja na
mipangoz mizuri ya serikali lakini bado wazee wanakabiliwa na baaadhi ya changamoto
ikiwemo wazee kubebeshwa tuhuma za uchawi ndani ya jamii, uchakavu wa majengo
wanayoishi wazee, Pamoja na kuanywa nyuma katika utekelezaji wa baadhi ya
mipango ya kisekta.
Aidha, katika risala
hiyo, wazee waliishauri serikali kushusha umri wa wazee katika kuopkea pencheni
jamii ili iweze kutoa fursa kwa wazee wengi Zaidi waweze kupata penchini
hiyo Pamoja na kuanzishwa kwa dirisha maalum katika vituo vya Afya kwa ajili ya
kuwahudumia wazee.
Nae, Mkurugenzi wa
Shirika la kuwahudumia wazee Duniani nchini Tanzania (Help Age
International) Smart Daniel Alipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa
kuanzisha program maalum ya pencheni jaamii jambo ambo limepelekea baadhi ya
nchi katika bara la Afrika kuiga jambo hilo ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda kwa
upande Nchi za Afrika Mashariki.
Alieleza, kauli mbiu
ya mwaka huu inalenga kuwashirikisha wazee katika kuchangia pato la taifa hasa
katika matumizi ya kidigitali.
Kauli mbiu ya mwaka
huu ni “MATUMIZI SAHIHI YA KIDIGITALI KWA USTAWI WA RIKA ZOTE”.
0 Comments:
Post a Comment