| Salum Vuai Issa9Muhenga) |
Salum Vuai
MIAKA kadhaa iliyopita, mimi na mpiga
picha wangu tuliwahi kulitembelea eneo la Mpigaduri karibu na skuli ya
maandalizi Saateni Wilaya ya Mjini.
Wakati huo ndio kwanza watu walikuwa
wameanza kulivamia eneo hilo na kukatiana au kugaiana viwanja kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba za makaazi.
Katika hali ambayo hatukuitarajia,
tulikuta mikoko mingi imekatwa kupisha ujenzi wa nyumba za tofali tena zilizoezekwa
bati kama kwamba eneo hilo limehalalishwa na mamlaka zinazosimamia ardhi
nchini.
Tulipiga picha nyingi na kuzitumia katika
gazeti la Zanzibar Leo kwa lengo la kuziamsha mamlaka zenye dhamana ya ardhi,
mipango miji na mazingira tukiamini pengine hazikuwa na habari juu ya
kinachoendelea mikokoni humo.
Kumbe kitendo hicho hakikusaidia chochote
na niseme tu ilikuwa kama tumewachonga watu ukali.
Watu waliendelea kujimilikisha maeneo hayo
hadi yakageuka mtaa mpya, ambao bila shaka unapata baraka zote za taasisi
nyengine kwani huduma za umeme na maji zinapelekwa na watu wanaishi raha
mustarehe.
Kwa hakika hii inashangaza kwani katika
hali ya kawaida, Tafakuri isingetarajia watu wakatiwe viwanja, kujenga nyumba
na kuanzisha makaazi kwenye maeneo hayo.
La kushangaza zaidi, haya yanafanyika
katika eneo ambalo liko karibu kabisa na idara ya Mazingira Maruhubi. Je,
wahusika hawana habari?
Kwa watu wenye umri kuanzia miaka 50 na
kuendelea ambao wanalijua vyema eneo hilo na mitaa inayolizunguka, watakuwa
wanaelewa vyema kwamba katika miaka ya nyuma sehemu hiyo ilikuwa na mandhari
nzuri kwa vile maji ya bahari yalipojaa yalifika hadi huko kulikojengwa sasa.
Sote tunafahamu kuwa, endapo mtu anahitaji
ardhi kwa ajili ya ujenzi, anapaswa kufuata taratibu za kisheria kwa kupitia
ngazi husika zinazohusisha halmashauri za miji, masheha na Idara ya Ardhi na
Upimaji.
Lakini kwa hali inavyoonekana, eneo hilo,
ama watu wanajichukulia tu kama matunda pori yasiyokuwa na mwenyewe baada ya
kuzungumza vizuri au wanauziana kinyume na sheria.
Yumkini haya yana mkono wa wenye dhamana
ambao nao bila shaka wananufaika kwa njia moja au nyengine.
Ujenzi huu ni tishio kubwa la kimazingira
katika kipindi hichi ambacho binadamu anaendeshwa zaidi na utashi wa nafsi
yake, na kamwe hafikirii athari zinazoweza kutokea kwa nchi endapo atapuuza
umuhimu wa kutunza mazingira na rasilimali za taifa.
Kwa hili, ndipo ninapoona kuwa tatizo la
uharibifu wa mazingira halitokani na kile kinachoitwa mabadiliko ya tabianchi,
bali husababishwa na 'Tabiawatu'.
Wakati viongozi mbalimbali pamoja na
wanaharakati wa masuala ya mazingira, wakiendelea kufanya mikutano na warsha za
kila mara zinazogharimu fedha nyingi, kujadili na kuweka mikakati ya kupambana
na mabadiliko ya tabianchi, wanasahau kwamba kinachotuumiza ni tabia za watu
wasiojali na ambao hawataki kubadilika.
Ni kweli kwamba mabadiliko ya hali ya hewa
yamekuwa yakisababisha athari nyingi katika jitihada za binadamu kujitafutia
maendeleo, lakini kiumbe huyo huyo ndiye sababu ya majanga hayo.
Kwa kuwa utashi wa binadamu ndio
unaowafanya wavamie rasilimali na maliasili za baharini na misituni na
kuzihujumu, iko haja kwa wataalamu wa mazingira, walione pia tatizo la ‘TABIAWATU’.
Viongozi, wanaharakati na wadau wa
mazingira wataendelea kupiga kelele kwa kulaumu tabianchi, lakini wafahamu
kuwa, mikono ya watu ndiyo adui mkubwa wa janga la kimazingira linalozinyemelea
nchi zetu hasa hapa Zanzibar.
Kama sheria za kulinda na kuhifadhi
mazingira zipo, kwa nini watu wanazivunja na wanaonekana lakini hakuna hatua
zinazochukuliwa dhidi yao?
Bila shaka, wanaovunja sheria hizo,
wanapata jeuri kwa kuwa wanabebwa na kukingiwa kifua na baadhi ya watendaji wa
ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuzisimamia.
Kumbe tulikuwa tunasubiri ziara ya
kiongozi wa juu katika eneo hilo ndipo waliopewa dhamana wazinduke na kujua
athari inayoitafuna nchi?
Tutarajie ziara ya Makamu wa Pili wa Rais
huko Mpigaduri iwe chanjo ya kinga ya uzembe na utendaji kazi kimazoea ili
wananchi wasivuke mipaka ya uhuru walionao kwa kulazimisha mambo yasiyostahili
yanayoweza kuipeleka nchi katika janga na majuto ya milele.
Tuache kuangalia pale tulipoangukia,
badala yake tutazame wapi tulipojikwaa na kuchukua hatua muafaka kwa kubaini
vyanzo vya matatizo yanayoimaliza nchi yetu, ambavyo kukabiliaana navyo
kunahitaji zaidi vitendo na sio mdomo mtupu.
Simu: 0777 865050/0714 425556
Baruapepe: salumss@yahoo.co.uk.

0 Comments:
Post a Comment