Mkakati wa kuwarudisha waliotoroka Skuli waanza vyema Micheweni


Jumla ya wanafunzi elfu moja miamoja na kumi na nane  kati ya  wanafunzi Elf saba miasita ambao waliripotiwa kukatisha masomo kwa utoro katika wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba tayari wameanza kurudi  katika skuli zao  katika maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.

Akizungumza na habari hizi mkuu wa wilaya ya micheweni  Mgeni khatib Yahya amesema juhudi hizo ni mashirikiano yake na  wizara ya elimu kisiwani pemba katika kulisimamia suala hilo   kwa wanafunzi hao.

Amesema kuwa   idadi hiyo  itaendelea kuongezeka siku hadi siku  mpka pale watakaporejea wanafunzi wote  kwani tayari wizara ya elimu inafuatilia suala hili ili kufanikisha taratibu za watoto hao kurudi skuli.

 Alieleza kuwa wimbi hilo la wanafunzi ambao walikuwa hatarini kukatisha masomo kutokana na utoro lilisababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo ajira za watoto katika wilaya hiyo, ambapo tayari uongozi wa wilaya unaendelea kulidhibiti suala haraka katika maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.

 Aidha ameeleza kuwa   wilaya hiyo  imejiwekea mikakati madhubuti ili kuona watoto wote wanapata haki yao ya msingi ya kupata elimu  kwa wale ambao wamekatisha masomo na wale ambao hawajaandikishwa  waweze kupata haki yao ya lazima

Alieleza kuwa  serikali  ya wilaya tayari imeanza  kuwapa  onyo wale wote ambao wanatoa ajira kwa watoto ikiwemo kuwaanikisha madagaa, kupara samaki ndani ya Bandari  kuacha mara mija tabia hiyo hatarishi kwa watoto.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment