| Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdallah |
r.
Mhe. Hemed alitoa witò huo wakati akilifungua kongamano la wadau
wa utalii Zanzibar lililofanyika katika Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar.
Aliwashauri wadau hao kubuni mbinu mpya zenye kuzingatia
ushindani kwa kuibua vivutio vipya sambamba na kuviimarisha vivutio vyengine
ili viwe na mazingira yatakayowashawishi watalii kurudi tena kuitembelea
Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais aliwaomba wadau wa utalii kutorizike na
dhana kuwa Zanzibar inajitangaza yenyewe bali inapaswa kuchukua jitihada za
maksudi ili kuingia katika ushindani kutokana na nchi nyengine kuendelea kuchukua
hatua mbali mbali za kutangaza nchi zao.
Aidha, Mhe. Hemed aliupongeza uongozi wa Jumuiya ya Kitaifa ya
wafanyabiashara Zanzibar kwa kushirikiana na UNDP kwa hatua wanazozichukua
katika kurudisha ustawi wa sekta ya utalii Zanzibar kwa ajili kuinua uchumi wa
Nchi.
Alisema sekta ya utalii Zanzibar iliathiriwa na maradhi ya
UVIKO-19 ambapo ikekuwa ikitegemea kwa asilimia kubwa ya ukuaji wa uchumi wake
kupitia sekta ya hiyo.
Alieleza kuanguka kwa Soko la utalii Zanzibar kulipelekea
kusimama kwa ajira nyingi za wanachi kulikosababishwa na kufungwa kwa hotel
jambo lililopelekea kushuka kwa pato la serikali kwa ajilibya kutoa huduma
msingi kwa wananchi wake.
"Athari za UVIKO-19 kumesababisha kushuka kwa ukushanyaji
wa mapato jambo lililoathiri utoaji wa Huduma kama vile maji safi, ukarabati wa
miundombinu ya Barabara" Alieleza Mhe. Hemed
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais alikemea vikali
tabia inayofanywa na baadhi ya watembeza watalii kwa kuharibu viumbe hai vya
baharini ikiwemo STAR FISH hali inayopelekea kuharibu rasilimali za bahari.
Nae, Waziri wa Utalii na mambo yakale Mhe. Lela Mohamed Mussa
alisema wizara imekuwa na utamaduni wa kushirikiana na wadau tofauti katika
kufufua utalii ulioathiriwa na maradhi ya UVIKO-19.
Alieleza kuwa, kutokana na maradhi ya UVIKO-19 kuikumba dunia
imesababisha Jumuiya za kikanda ikiwemo Afrika Mashariki na SADC kuwa na vikao
vya pamoja katika kujadili na kutathmini namna bora ya kufufua utalii katika
nchi zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya kitaifa ya
wafanyabiashara Zanzibar Ali Amour alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa
katika mwaka 2020 sekta ya utalii ilitarajiwa kuchangia pato la taifa (GDP) kwa
asilimia Thelasini na Tano (35%) pia ilitarajiwa kukusanya asilimia Themanini
(80%) ya mapato pamoja na kuajiri watu wapatao laki moja (100,000) lakini
kutokana na janga la UVIKO-19 lilisababisha kushindwa kufikiwa kwa lengo hayo.
Nae, Mwakilishi kutoka UNDP Madam Rukia Wadoud alisema UNDP
inaipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wake inautoa kwa
kuwashirikisha wadau kutoka taasisi binafasi na kuahidi kuwa UNDP itaendelea
kutoa ushirikiano wake kwa serikali ili kuinua maendeleo ya sekta ya utalii Zanzibar.
0 Comments:
Post a Comment