Mke wa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan amesema kuna kila sababu ya
kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan juu ya azma alionayo ya kuimarisha uchumi wa Nchi.
Mama Sharifa Omar
alieleza hayo katika kilele cha matembezi ya mshikamano ya kumuunga mkono
mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Samia Suluhu Hassan mataembezi ambayo yaliyoanzia kibuteni na kumazia
kizimkaazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mama sharifa alieleza
kuwa, wanachama wa chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla wana kila sababu
ya kumuunga mkonoi Rais Samia kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya
kuiongoza nchi ikizingatiwa kasi alioanza nayo ya kuwaeletea maendeleo wananchi
wa Tanzania ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Aidha, mke huyo wa
Makamu wa Pili wa Rais alisema ipo haja ya umoja wa wanawake mkoa wa
kusini kuungana Pamoja na kauli ya mwenyekiti wa CCM taifa ya kumuweka
madarakani mwanamke kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo mwaka
2025.
Pamoja na mambo
mengine Mama Sharifa Khalfan aliwaeleza Umoja wa wanawake Mkoa wa Kusini kuwa
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi
anawaunga mkono na anawataka wanachama katika Mkoa huo kufanya kazi kwa umoja
na mshikamano ili kuweza kuiletea maendeleo Zanzibar na Tanazania kwa Ujumla.
Akisoma risala ya Umoja wa wanawake wa Mkoa wa kusini
Unguja katibu wa UWT wa Mkoa huo Asha Mzee Omar amesema uongozi wa
UWT Mkoa wa Kusini umeona ipo haja ya kuuanda matembezi hayo yenye azma
ya kumpongeza mwenyekiti wa chama Taifa kutokana na mwanzo mzuri wa
utendaji wa kazi zake kwa kuisimamia demokrasia na kuwajali wananchi
wanyonge.
Aidha Katibu Asha amesema kuwa, kufuatia fedha
zililizoelekezwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambae pia ni Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan katika ngazi zote za
halmashauri zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha miundombinu yan chi
sambamba na kupambana na maradhi ya UVIKO-19.
Nae Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja
Shemsa Abdalla Ali amemuelezea Rais Samia kuwa ni kiongozi mwenye maono na
kipaji cha uongozi kutokana na umahiri wake ndani ya kipindi cha muda mfupi
ameanza kuonesha dira na mueleko chanya wa taifa la Tanzania.
Katika Hatua nyengine Mwenyekiti Shemsa Abdalla
ametumia fursa hiyo kwa kuwashajihisha wanachi kuendelea kujitokeza kwa wingi
kupata chanjo ili kujikinga na maradhi ya UVIKO- 19 ambayo yamekuwa
tishio Tanzania na duniani kwa ujumla.
Mapema Mama Sharifa Omar Khalfan amepokea matembezi ya
kumuunga Mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan yalioanzia Kibuteni
na kumalizia Kizimukazi.
0 Comments:
Post a Comment