
Katibu Mkuu OMKR Dkt Omar Dadi Shajak akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa ndani wa OMKR katika ukumbi wa mkutano Migombani Zanzibar
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Dkt Omar D. Shajak amehimiza mashirikiano katika kutekeleza
majukumu ya kazi jambo ambalo litasaidia kutoa maamuzi sahihi ya kiutendaji
hasa kwenye masuala yanayohusu ukaguzi wa hesabu za ndani.
Dkt Omar D. Shajak ameyasema hayo
wakati akizindua kamati ya Ukaguzi wa ndani ya Ofisi hio iliyofuatiwa na
mafunzo kwa wajumbe hao, kwenye ukumbi wa mkutano wa Migombani na kuwataka
wajumbe wa kamati hio kuhakikisha wanatoa ushauri unaofaa kwenye masuala ya
matumizi ya fedha.
Amewakumbusha wajumbe hao kuwa lengo
la kuundwa kwa kamati hio ni kuzipitia kwa kina na kuzifanyia kazi hoja
zitakazojitokeza kwenye taarifa ya mkaguzi na kufanya maamuzi sahihi ya taarifa
hio kwa vile moja kati ya jukumu lao ni kumshauri msimamizi mkuu wa fedha ndani
ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Dkt Shajak amesema Kamati ya ukaguzi
imeundwa kisheria ili kuhakikisha matumizi yote yanafanyika kama ilivyokusudia
“nyinyi mtasaidia kunyoosha utaratibu na kama kuna dosari muweze kuzianisha ili
kuepusha kukiuka taratibu zilizowekwa” alisisitiza Dkt Shajak.
Aidha amewasisitiza fedha ya
serikali inatakiwa kutumika kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kuepusha
matumizi yaliyo nje na utaratibu pamoja na kuhakikisha hoja zitakazoibuliwa na
mkaguzi wa ndani zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Akitoa sifa za mjumbe wa Kamati ya
Ukaguzi mkufunzi wa mafunzo Bi Safia Zubeir kutoka Wizara ya Ujenzi Mawasiliano
na Uchukuzi amesema wajumbe wa Kamati ya ukaguzi ili waweze kufanya kazi vyema
na kutoa maamuzi sahihi anatakiwa kuwa muadilifu, muwajibikaji, mwenye uwezo wa
kupima na kushauri.
Pia amesema uadilifu unakufanya kuwa
mwaminifu na kuaminika katika majukumu ya kazi, kujali muda mambo ambayo
yanasaidia kuifanya kamati kuwa imara na kuwa tayari muda wote kufanyakazi kwa
ajili ya kumsaidia Katibu Mkuu ili kuwezesha kufanikiwa majukumu na malengo
waliyojipangia kwa wakati.
Wajumbe wa Kamati hio wamejifunza
maadili ya kazi na majukumu ya kamati, sifa zake, faida ya kuwepo kamati ya
ukaguzi na changamoto ambapo mkufunzi huyo amesisitiza haja ya wajumbe wa
kamati hio kujengewa uwezo ili kuelewa vyema majukumu yao na kuyatekeleza
kitaalamu zaidi .
Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani wa
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Maryam Rajab Baraka na kwa niaba ya kamati
hio ametoa shukurani kwa Katibu mkuu kufuatia kuunda kamati ambayo ipo kwa
mujibu wa utaratibu wa sheria
0 Comments:
Post a Comment