| Picha na Maktaba |
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haji Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito
kwa waislamu kujitokeza Zaidi kusaidia harakati za kuunga mkono masuala ya dini
ili kuijenga jamii yenye maadili mema.
Makamu wa Pili wa Rais
alieleza hayo wakati akimuwakilisha Rais Dk. Mwinyi wakati akifungua rasmi
masjid Muhamad Khaula Alqaaz uliopo Kisauni Wilaya ya Magharibi “ B” Unguja.
Mhe. Hemed aliwataka
wasimamizi wa Masjid Muhamad katika kuendesha mskiti huo kuna haja ya kutoa
mafundisho mema kwa vijana yatakayowajenga kifikra, kitabia na kiakhlaki kwa
lengo kufikia lengo lililokusudiwa.
Aliwakumbusha viongozi
kuutunza mskiti huo sambamba na kuendeleza Amani, Utulivu na mshikamano
miongoni mwa waumini jambo litakalosaidia kustawisha Imani na maenedeleo
Nchini.
Aidha, Makamu wa Pili
wa Rais aliwahakikishia waumini hao kuwa Rais Dk. Mwinyi ataendelea kutoa
ushirikiano kwa kuzingatia taratibu na miongozo katika kuendeleza mskiti huo.
Nae, Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume aliwataka waumini hao kuepuka migogoro isiokuwa
na tija katika uwendeshaji wa mskiti huo.
Sheikh Khalid alisema
mskiti ni nyumba ya M/mungu hivyo ofisi ya Mufti haitapenda kuona katika nyumba
hiyo kunajitokeza mizozo itakayosababisha mitafaruki miongoni mwa waumini.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Islamic Foundation Samahatu Sheikh Arif Naad alisema taasisi hiyo
itaendelea kutoa ushirikiano wake katika kuendesha harakati za kuhuwisha huduma
za jamanii ikiwemo ujenzi wa miskiti pamoja na huduma nyengine muhimu.
Sheikh Arif Naad
aliomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuipatia taasisi hiyo eneo maalum kwa
ajili ya kujenga Ofisi zake zinakazopelekea kufanya kazi zake kwa ushirikiano
wa karibu na Ofisi ya Mufti Zanzibar.
Mapema Mhe. Hemed
alijumuika pamoja na waumini wa Masjid Muhamad Khaula Alqaaz katika ibada ya
sala ya Ijumaa.
0 Comments:
Post a Comment