| Muonekano wa mji wa Chakechake mkoa wa kusini Pemba |
Baadhi ya watu wenye ulemavu wilaya ya
Chake chake, wamependekeza kuwa, kituo cha chanjo dhidi ya UVIKO 19, kiondolewe
kilipo sasa, kwenye jengo la ghorofa moja la Hospitali ya Chake chae, na
kishushwe chini ili kuwarahisishiya wanaotaka huduma hizo.
Walisema, kwa watu
wenye ulemavu na hasa wa viungo na macho, imekuwa tatizo kuzifikia huduma za
chanjo na kusababisha usumbufu kwao.
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi, walisema kwa wenzao wenye ulemavu kama miguu na macho
ni tatizo wanapotaka huduma hiyo.
Mmoja kati ya watu
wa kundi hilo, Amiri Haji Amiri mwenye ulemavu wa viungo, alisema hakuna hata
mmoja wao anaweza kufizifikia huduma za chanjo, zilizopo hospitali ya Chake
chake.
Alisema, kwa vile
pana ngazi mbili kabla ya kuzifikia, inaweza kuwa kikawazo chengine kwao,
kuzifikia huduma hizo ambazo nao ni haki yao kiafya.
“Ni vyema mamlaka
husika kuangalia kuzihamisha huduma za chanjo hospitali ya Chake chake, maana
ziko juu na sisi wengine hali yetu ni ya ulemvu, inatubidi tubebwe,’’alieleza.
Khadija Hassan
Omar, alisema wakati mumefika kwa tasisi hasa za umma, kuzingatia majengo
rafiki kwa kundi la watu wenye ulemavu, wawe sawa na wengine.
Alieleza kuwa,
mfano wa huduma hizo za chanjo ni jambo moja, ingawa zipo huduma nyingine,
katika ofisi za umma nazo watendaji wako juu.
“Unakuta jengo
linaghorofa zaidi ya moja, kisha hakuna ngazi mwendo ‘lift’ na pengine msemaji
kuu ndio amechangua chumba kilichoko juu, hii sio haki kwetu,’’alilalamika.
Mjumbe kutoka
Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar ‘UWZ’ ofisi ya Pemba Hidaya Mjaka Ali,
alisema suala la chanjo ya UVIKO -19 ni haki ya makundi yote.
Alieleza kuwa, ili
kufikia hilo, ni vyema kwa wizara ya Afya kuzingatia jengo na eneo
zinapotolewa, ili zisiwe chanzo cha ugumu kwa kundi la watu wenye ulemavu.
Akizungumzia hilo,
Mratibu wa maradhi yanayoambukiza Pemba Khamis Bilali, alisema kwanza kutokana
na miundimbinu ya jengo lao, kwasasa ni vigumu kulibadilisha.
Alisema utaratibu
wao ni kuwafuata wenye mahitaji maalum kwa kushuka madakatari chini na
kuwapatia huduma za chanjo, iwe ni wenye ulemavu au wagonjwa wengine.
“Ni kweli kwa sasa
eneo ambalo tumeliteua kwa ajili ya chanjo UVIKO-19, ndani ya hospitali ya
Chake chake, inabidi mwenye kuhitajia apandishe ngazi mbili, lakini akiwa
hawezi madaktari wanamfuata alipo.
Katika hatua
nyingine, Mratibu huyo alisema, kama kundi la watu wenye ulemavu na
wameshajikusanya pahala, Idara yake itawafuata kuwapa huduma hiyo popote walipo.
“Chamsingi
wajikusanye na kuwasiliana na sisi Idara ya chanjo, watu hao wenye ulemavu au
mahitaji maalum, ili wasipate usumbufu, bali sisi ndio tutawafuata hata kama
visiwani,’’alifafanua.
Hata hivyo
aliwataka wananchi kuendelea kuitumia fursa hiyo ya chanjo na hasa kwa vile ni
bure, na waondoe dhana iliyopo kuwa chanjo hiyo ni hatari kwao.
“Jamani serikali
yetu inawapeda mno watu wake, hivyo kweli ipokee chanjo ambayo inaathari, na
kisha iwatake hata madaktari wake wachome chanjo hii,’’alifafanua.
Zoezi la uzinduzi
wa chanjo ya UVIKO -19 kwa kisiwani Pemba lilizinduliwa rasmi Augosti 27, mwaka
huu katika hospitali za Micheweni, Wete, Mkoani na Chake chake Pemba.
0 Comments:
Post a Comment