Polisi yawanawasa wawili na kete 350 za heroin Pemba

 


Na Amina Ahmed

aahmed@marhabanews.net

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limefanikiwa kukamata jumla ya kete 350 zinazodaiwa kuwa ni  madawa ya kulevya aina ya heroini sambamba na kuwashikilia watu wengine ambao wanadaiwa kuhusika na biashara hio.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba ACP Richard Tadei Mchovu amewataja waliokamatwa na madawa hayo kuwa ni Ali Mjawiri mwenye umri wa miaka 40 mkaazi wa Madungu ambaye alikamatwa maeneo ya Africana   na mwengine ni Said Moh`d (30) mkaazi wa Minazini Chake Chake ambao wote wawili wamekamatwa kwa tuhuma za aina moja.

Kamanda huyo pia aliitaka jamii kisiwani humo kutowafumbia macho watu wanaodhani wanahusika na uingizaji,usambazaji n ahata matumizi ya dawa za kulevya na kuwataka kutoa taarifa katika vyombo husika ili waweze kuchukuliwa hatua.

Aidha Kamanda Mchovu amesema katika operesheni ya usalama barabarani wiki hii jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba imekamata jumla ya pikipiki 65 kwa makosa mbali mbali ikifemo kutokuwa na leseni, bima, na makosa ya kutovaa helment kwa madereva na abiria ambapo  baada ya kufikishwa mahakanai baadhi ya maderva wa vyombo hivyo wamelipa faini na  ambapo jumla ya shilingi milioni moja laki tatu na elfu 20  elfu zimepatikana.

 

Hata hivyo kamanda huyo amesema operation hizo mbili ni endelevu ambazo lengo lake  ni kumaliza  vitendo viovu  katika mkoa huo.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment