Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima leo amemtembelea Mama Zaina Khamis mwenye Watoto sita waliokosa fursa
ya kupata elimu ingali umri wao wanastahili kuendelea na masomo anaeishi na
wanae katika kata ya Bangulo Gongo la mboto, Jijini Dar es Salaam.
Familia hiyo ilikuwa ikiishi Tabata Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam
kabla ya kutelekezwa na kuamia Bangulo ili kupata hifadhi katika kipindi hiki
wanachopitia hali ngumu ya maisha na changamoto ya uhusiano wa kifamilia.
Akiongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Dkt. Mfaume pamoja
na Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Mkoa Dkt. Gwajima ameagiza familia
hiyo kupewa hifadhi katika makazi ya kulelea Watoto wenye uhitaji, huku
taratibu za kuwapeleka shule Watoto wote zikiendelea.
Pia, amewaagiza Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kufuatilia mzazi mwenza
wa Mama Zaina ili kujua ukweli kuhusu jambo hilo ikibidi kutatua changamoto zao
ili kuinusuru familia hiyo.


0 Comments:
Post a Comment