Wananchi Pemba waiomba Serikali kuongeza nguvu zaidi vita dhidi ya udhalilishaji




Na Amina Ahmed,Pemba

aahmed@marhabanews.net

Wananchi katika shehia ya Wara Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wameiomba serikali kuzidisha nguvu ya kupambana na vitendo viovu vinavyochangia kuharibika kwa maadili ya jamii na kupelekea kuongeza matendo ya udhalilishaji wa wanawake na watoto.

Ombi hilo wamelitoa katika mkutano maalum ulioandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Vijana Pemba juu ya kuelimisha na kupata maoni ya wananchi njia bora zitakazosaidia  kudhibiti  kutokomeza vitendo vya udhalilishaji.

Wamesema katika shehia hiyo ya Wara kuna baadhi ya  nyumba ambazo zilimekodisha kwa ajili ya makaazi ya watu lakini wapo wengine huzitomia vibaya kwa kudhalilisha  mabinti jambo ambalo limekuwa likizidi kuporomosha maadili ya watoto.

Naye Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mendeleo ya Vijana Pemba Khamis Juma Khamis amesema lengo la kufanya mikutano ya shehia mbali mbali ni kuisadiia serikali katika vita ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji na mmong`onyoko wa maadili.

Kwa upande mlezi wa Jumuiya hiyo Pemba Hafidh Abdi Said ametoa wito kwa akinamama wa shehia hiyo kuwa mstari wa mbele kupaza sauti zao kwani wao ndio wahanga wakubwa katika matendo ya udhalilishaji.

Jumuiya ya Maendeleo ya Vijana Pemba imedhamiria kuwafikia wananchi katika shehia mbali mbali ili kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, utumiaji wa madawa ya kulevya na mmong`onyoko wa maadili kwa vijana na jamii kwa ujumla

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment