
Na.Catherine Sungura,Dodoma
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wametakiwa kujifunza kuhusu Masuala ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ili kuweza
kuwafafanuliwa wananchi wao.
Hayo yamesemwa leo na Dkt.Tulia
Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa
semina ya wabunge kuhusu Corona iliyoandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
Akiongea wakati wa semina hiyo
Dkt.Tulia amesema Kuwa Wabunge Kama wawakilishi wa wananchi nafunzo hayo ni
Furaha Kwao kujifunza masuala ya ugonjwa huko ikiwemo uvaaji sahihi wa barakoa
na umuhimu wa Chanjo.
“Sisi wabunge ambao ni wawakilishi wa
wananchi mafunzo haya ni Fursa kwetu ya kujifunza kuhusu masuala ya UVIKO-19
ikiwemo uvaaji sahii wa barakoa na umuhimu wa kuchanja”Alisema
Dkt.Tulia aliongeza kuwa wanalo
jukumu kila mmoja la kujifunza zaidi ili kuweza kusaidia jamii kuondokana na
upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwenye maeneo Yao.
Hata hivyo Naibu Spika huyo alisema
wataendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa Chanjo,uvaaji
sahihi wa barakoa na afua nyingine za kujikinga kwani wamejengewa ujasiri wa
nini waongee kwa wananchi.
Wakati huo huo Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima alisema kuwa
hawajazifuta Tiba asili/mbadala bali wao Kama Serikali wanazibeba afua zote
mbili ya Tiba asili na Chanjo ya UVIKO-19.
“Hatujazifuta Tiba asili katika
kukabiliana na ugonjwa huu,tiba asili ni matibabu wakati tayari unaumwa Ila
Chanjo ni kinga ya usiambukizwe au ukiambukizwa ugonjwa uwe mwepesi”Alisisitiza
Dkt.Gwajima alisema Kama Wizara
wamejipanga kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga na utoaji
wa Chanjo kwa kila Halmashauri kwa kushirikiana na TAMISEMI.
Naye,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo alisema kuwa
ujumbe Mkubwa ni kwamba Mtu ambaye hatochanjwa yupo katika hatari kubwa zaidi
pindi atakapopata ugonjwa huo.
Mhe.Nyongo amempongeza Waziri wa Afya
kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendelea kupambana kwa kutoa elimu ya
kujikinga kwa wananchi.
0 Comments:
Post a Comment