Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akisistiza jambo katika moja ya kazi zinazofanywa na chama hicho.Picha kwa hisani ya maktaba.
Chama
cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kinaviomba
vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa
waliohusika na vitendo vya upigaji na uuaji wa wanawake na watoto vilivyotokea
hivi karibuni, hapa Zanzibar.
Hivi
karibuni msichana wa miaka 23 Sumaiya Mohammed Said mkaazi wa Jambiani Kikadini
mkoa wa kusini Unguja amedaiwa kuuwawa kwa kupigwa mapanga na Imani Abdallah Abdallah umaarufu Kichele (38).
Tukio
jengine la ukatili dhidi ya wanawake lilitokea huko Fuoni nyumba moja mkoa wa
Mjini Magharibi, Unguja ambapo bi Raya
Khamis Mgeni (45) alidaiwa pia kushambuliwa kwa mapanga yeye na mtoto wake aliye chini ya mwaka mmoja.
Mashambulizi
hayo yalipelekea kifo cha mtoto huyo asiye na hatia na kumjeruhi vibaya Bi Raya
ambaye amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja tokea tarehe ya tukio,
30/8/2021.
Kwa
mujibu wa rikodi za TAMWA ZNZ tangu mwaka 2016, matukio 19 ya mauwaji ya
wanawake na watoto yameripotiwa (wanawake 15 na watoto wanne) ambapo ni matukio
machache tu ndiyo yaliyofikishwa katika
Mahakama Kuu ya Zanzibar yakiwemo ya Wasila Mussa (21) na Hajra Abdallah
Abdallah (21).
Hivyo,
TAMWA-ZNZ inaviomba sana vyombo vya ulinzi kukomesha vitendo hivi kwa
kuwatafuta wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wapewe adhabu
inayowastahiki.
Hali
ya kuvamiwa wanawake na watoto na kupigwa inavunja haki ya msingi ya wanawake
ya kuishi kwa amani na pia inawatia hofu katika kuendeleza shughuli zao muhimu
za kimaendeleo.
0 Comments:
Post a Comment