Mratibu eneo la kutotolea vifaranga vya samaki
Khamis Hassan Ali (katikati) akiwapatia maelezo wadau wa (IORA) kuhusiana na
uzalishaji wa vifaranga aina mbalimbali ikiwemo sato,kambare,kaa ,majongoo na
matiko katika eneo hilo liliopo Beit-Ras kibweni Mjini Unguja.
Wadau wa jumuiya ya nchi zilizopo kwenye mwambao wa bahari ya hindi wametakiwa kuzitangaza fursa zilizopo nchini ili kuimarisha uwekezaji katika sekta ya uvuvi.
Agizo hilo limetolewa
na Katibu Mkuu Ikulu, Mussa Haji Ali wakati akifunga kikao cha siku tatu cha
wadau wa jumuiya hizo katika kika kilichofanyika katika Ofisi za ZURA Maisara
Mjini Unguja.
Alisema fursa zilizopo
katika bahari ya Hindi ni nyingi ikiwemo uwekezaji katika sekta ya uvuvi wa
bahari kuu ambao unaleta faida kubwa katika kukuza uchumi wa buluu nchini.
Alieleza kuwa,
Serikali inatambua umuhimu wa jumuiya ya nchi zilizopo kwenye mwambao wa bahari
ya hindi hasa katika kuutangaza utalii ambao unasaidia katika kukuza uchumi wa
taifa.
Alisema Serikali zote
mbili zinaendelea kufanya jitihada za kuimarisha matumizi bora ya bahari
ikiwemo kupiga vita uvuvi haramu katika bahari ili kulinda uchumi wa bahari.
Aidha katibu huyo
alisema ziara zilizofanywa na wadau hao ya kutembela kituo cha kutotolea
vifaranga Kibweni na Mamlaka ya bahari kuu Fumba ziwe ni chachu ya kuibua
mawazo mazuri yatakosaidia katika kufanikisha uchumi wa buluu nchini.
Mapema Naibu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu, Dk. Emmanuel Sweke ameswema ipo
haja ya kuwahamasisha wazawa kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu ili rasilimali
za taifa zitumike kuwanufaisha wananchi.
Alifafanuwa kuwa
wawekezaji wengi wanaokuja kuwekeza katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu ni
wageni, hivyo ipo haja ya kuwawezesha wazawa kimtaji ili waweze kuwekeza.
Aidha alipendekeza
ujenzi wa bandari ya uvuvi nchini,ujenzi wa viwanda vya samaki,upatikanaji wa
boti, na ufugaji wa samaki ufanyike nchini ili rasilimali ya bahari ilete manufaa
makubwa zaidi kwa taifa na kuzalisha ajira kwa watanzania.
Wadau wa jumuiya ya
nchi zilizopo kwenye ukanda wa bahari ya hindi walipata fursa ya kutembelea
kituo cha kutotolea vifaranga vya samaki Kibweni na Mamlaka ya Uvuvi wa bahari
kuu Fumba.
0 Comments:
Post a Comment