Na Amina Ahmed,Pemba
aahmed@marhabanews.net
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali kisiwani pemba ili kukuza biashara zao na kujipatia kipato .
hayo ameyasema mkuu wa mkoa wa kusini pemba Matar Zahor Masoud katika mafunzo ya ya siku moja ya wajasiriamali yalioandaliwa na benki kuu ya Tanzania b o t pamoja na ofisi ya rais fedha na mipango zanzibar huko katika ukumbi wa ofisi hizo gombani chake chake pemba.
Amesema tayari serikali ya Mkoa huo inaendelea kuboresha miundo ikiwemo milango kwa ajili ya Wafanya biashara itakayosaidia upatikanaji wa soko kwa urahisi kwa wajasiriamali.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Mdhamini ofisi ya Rais fedha na mipango pemba Abdul wahab Said Abuubakar amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha kielimu wajasiriamali kutunza fedha na kuweza kuzitumia kwa matumizi yanayotakiwa .
Akiwasilisha mada mchumi muandamizi kutoka bank ya tanzania B.O.T Yurick Mumburi amesema lengo la kuwekwa mada mbili zinazohusiana na fedha ni kusaidia wajasiriamali hao kujua hali ya uwekaji na uingiaji fedha katika biashara zao.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kupitia mafunzo hayo kutawafanya kuweza kufanya matumizi kwa usahihi bila kuziharibu fedha zao ambapo wamesema awali walikuwa wanatumia fedha bila mipango maalum na kurudisha nyuma harakati zao za ujasiriamali.
Katika mafunzo hayo ya siku moja mada mbili ziliwasilishwa kwa wajasiriamali hao ni elimu ya fedha pamoja na usimamizi wa fedha na uwaandaaji wa bajeti.

0 Comments:
Post a Comment