Polisi Zanzibar wafunzwa sheria na haki za Binadamu

 





Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar limetakiwa kuendelea kulinda na kuheshimu kuheshimu misingi ya haki za binaadamu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi Zaidi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Bi Harusi Mpatani wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya siku moja kwa askari polisi juu ya haki za binadamu na umuhimu wa askari polisi kuziheshimu haki hizo, huko katika ukumbi wa chuo cha Polisi Ziwani, Mkoa wa Mjini MAgharibi Unguja.

Akiwasilisha mada ya Misingi ya haki za binadamu na makundi ya haki za binadamu, Bi harusi amewataka askari hao kuheshimu na kuilinda misingi hiyo katika utendaji wao wa kazi.

Aidha amewataka kuheshimu mipaka ya utendaji wao wa kazi, kama ilivyoainishwa na katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977.

“Uniform na silaha ni dhamana kwenu kwa hivyo hamutakiwi kukiuka sheria na kanuni za nchi zilizopo”alisema Bi Harusi kuwambia wanafunzi wa jeshi la polisi

Msimamizi wa mafunzo ambaye ni Mkuu wa utawala wa chuo cha polisi Ziwani, ACP Hasin Ramadhan Taufiq, akimwakilisha Mkuu wa Chuo ACP Augostino Senga amesema elimu ya sheria na haki za binadamu ni muhimili muhimu kwa jeshi la polisi katika kutekeleza vyema majukumu yao ya ulinzi wa raia.

“Sisi kama jeshi la polisi tunaamini kwamba mafunzo haya yanakwenda kuwa msaada mkubwa katika utendaji wetu wa kazi” alisema ACP Taufiq.

Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni askari wanaosomea cheo cha ukoplo, wamesema mafunzo hayo ni mazuri na yatawasaidia sana katika utekelezaji wa mjukumu yao.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kiutendaji ya kituo cha huduma za sheria Zanzibar (ZLSC) katika kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa kwa taasisi za serikali na zisizo za kiserikali na hasa kwa wasimamizi wa sheria wa jeshi la polisi na idara maalum za SMZ.

Amsema kwa sasa wanatarajia kufikia asakari elfu 3000 ambao watawapatia elimu ya sheria na haki za binadamu na wapo katika majadiliano kwa upande wa idara maalum za SMZ ili waweze kuwafikishia elimu hiyo.

Sambamba na hilo wanaendelea pia kuwafundisha wananchi mbali mbali kupitia vipindi vya televisheni na redio ili wajuwe umuhimu wa ulinzi wa haki za binadamu Pamoja na kuheshimu sheria.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment