RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga moto gari la Wagonjwa kabla ya kulikabidhi kwa Uongozi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba lililotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Pemba Mhe.Abdalla Hussein Kombo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo ilioko katika Wilaya ya Mkoani Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi ufunguo wa gari la wagonjwa Daktari Mkuu wa Mkoa (OMD) ambae pia ni Mkurugenzi Baraza la Mji Mkoani Dkt.Mohammed Faki Said ,kwa ajili ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, lililotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Pemba Mhe.Abdalla Hussein Kombo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo Mkoani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Mashine ya Kungolea Meno na Vifaa mbalimbali vya Afya kwa ajili ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba na Mfanyabiashara Maarufu wa Zanzibar Bw.Said Nassir Nassor (Bopar) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hospitali hiyo Mkoani Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na galoni la vitakasa mikono baada ya kukabidiwa na Mfaanyabiashara maarufu wa Zanzibar Bw.Said Nassir Nassor, na kukabidhi kwa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo imefanyika katika Hospitali hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba Dkt..Haji Mwita akitowa maelezo wakati akitembelea chumba cha X-Ray katika hospitali hiyo akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Vifaa mbalimbali vya Afya na Gari ya Wagonjwa kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo, wakati ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba
WAUGUZI wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Uongozi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba
WANANCHI wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kumaliza kukabidhi vifaa mbambali vya Afya na Gari ya Wagonjwa.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani
0 Comments:
Post a Comment