Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla
amesema serikali hatosita kumchukulia hatua mfanyabiashara yoyote atakaebanika kupandisha
bei za bidha bila ya kufuata taratibu kutoka taasisi husika kwa masla binafsi.
Hemed alileza hayo
wakati akitoa hotuba ya kuaghirisha Mkutano wa Nne wa baraza la Kumi la
wawakilisha katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Chukwani jijini Zanzibar.
Alisema, mbali na
sababu ya kupanda bei ya bidhaa katika soko la dunia lakini kumekuwepo na
vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa
waaminifu wanaosababisha kupanda kwa bei za bidhaa kunakosababishwa na
kuzingatia masalahi yao binafsi na kuacha kuwaangalia wananchi wanyonge.
Aliwataka
wafanyabiasha kuachana na visingizio visivokuwa na msingi vinavyopelekea
kupandisha bei kiholela bila ya kupata maelekeo kutoka Wizara ya Biashara na
maendeleo ya Viwanda.
Hemed aliendelea
kuuwagiza Uongozi wa Shirika la Bandari pamoja na taasisi ya viwango Zanzibar
(ZBS) kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria dhidi ya wafanyabiashara
wasiokuwa waaminifu na wanaoingiza bidhaa zilizo chini ya kiwango.
Aidha, Hemed alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya
baadhi ya watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu wanaoshiriki katika vitendo
viovu ikiwemo utoaji wa nyaraka, leseni na vyeti mbali mbali kwa kupatiwa watu
wasiostahiki kwa kutumia njia ya rushwa.
“ Spika Vitendo hivi
vinaitia aibu serikali na kusababisha lawama kwa wananchi wake” Alieleza Hemed ambaye ni Makamu wa Pili Rais Zanzibar.
Katika kuipatia
Ufumbuzi kadhia hiyo Makamu wa Pili aliwaagiza na kuwakumbusha viongozi wenye
dhamana kuacha mara moja kujihusisha na jambo hilo na badala yake wajitahidi
kuwasimamia watendaji walio chini ya dhamana zao ili kuwaondelea wananchi
usumbufu na kuhakikisha wananchi wote wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria na
taratibu zilizowekwa.
Akizungumzia suala la
miundombinu ya bara bara Makamu wa Pili wa Rais alisema serikali ilipanga
kujenga Jumla ya kilomita Mia mbili na Ishirni (220) za bara bara za ndani kwa
kiwango cha lami lakini kutokana na umuhimu uliopo serikali imeamua kujenga
Kilomita Mia mbili na Sabiini na tano (275).
“Pia serikali itajenga
kilomita Mia mbili na Ishirini na Moja (221) za bara bara kuu ambapo kwa
kipindi hiki tayari ujenzi wa barabara ya Wete Chake umeanza kwa hatua za
awali” Alisema Makamu wa Pili wa Rais.
Akiendelea na houtuba
yake, Mhe. Hemed alitumia fursa hiyo kuwakumbusha mawaziri, Wakuu wa Mikoa,
Wakuu wa Wilaya kufanya ziara na kuskiliza kero na malalmiko ya wananchi
ikiwemo migogoro ya ardhi inayoendelea kushika hatamu kila uchao.
Alieleza kuwa, ni
jambo linalosikitisha kuona changamoto ndogo ndogo za wananchi zinasubiri
kutatuliwa na viongozi wakuu wakati viongozi walipo katika ngazi mbali mbali
wana jukumu la kushugulikia changamoto hizo katika ngazi walizokuwepo.
Akigusia juu ya suala
la kilimo Makamu wa Pili wa Rais aliiagiza Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji,
Maliasili na Mifugo kukamilisha miradi waliyoianza na kuhakikisha Zanzibar
inajitosheleza kwa chakula kupitia sera na mikakti iliyopo.
Kuhu zao la karafuu
alifafanua kwamba serikali shirika la ZSTC wanaendelea na zoezi la kununua
karafuu ambapo hadi sasa nusu ya makadirio ya ununuzi wa karafuu
zimeshanunuliwa.
Vile Vile Makamu wa
Pili wa Rais ameonesha kusikitishwa kwake kutokana na taabia inayofanywa na
baadhi ya watu wanaouza karafuu katika shirika hilo la serikali kwa kuuingiza
vitu visivyohitajika katika bidhaa hiyo hali inayoplekea kuzichafua karafuu kwa
kuongeza vitu mbali mbali.
“Spika nakerwa sana na
changamoto iliopo ambapo baadhi ya watu wanaendelea kununua karafuu za wananchi
vijijini kwa kutumia vikombe, hapa natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na wilaya
pamoja na mashesha kutoa elimu kwa wananchi kwenda kuuza karafuu zao katika
shirika la ZSTC” Alieleza Hemed.
Akizungungumzia juu ya
mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) alisema mfuko huo unaendelea kuwa chahu ya
kuwasaidia wananchi walio maskini katika jamii ambapo serikali zote mbili zimo
katika utekelezaji wa kipindi cha pili cha mpango wa kunusuru kaya maskini.
Alieleza kuwa, Afisi
ya Makamu wa Pili wa Rais imendelea kuratibu kwa kuwarejesha katika mfumo wa
malipo kwa kaya 1,536 (Unguja 666 na Pemba 870) kutoka kaya 2,459 (Unguja 915
na Pemba 1,544) sawa na asilimia 62 za walengwa waliorejeshwa na asilimia 38 na
kaya zilizobakia ambazo zinaendelea kufanyiwa uhakiki wa kina.
Akizungumzia sekta ya
utalii Mhe. Hemed alieleza serikali imedhamiria kuendeleza sekta hiyo, kwa
kuchukua hatua mbali mbali ikiwemo kuansha mpango maalum wa kufufua utalii
(Torism Recovery Plan) mpango ambao umeanza kutoa matokeo Chanya kwa kuongezeka
kwa mashirika yay a ndege ya kimataifa kutoka Uholanzi na KLM la
Ujeruman.
Kwa upande wa maradhi
ya UVIKO-19 Makamu wa Pili wa Rais alieleza serikali inaendelea kuchukua hatua
madhubuti ya kujikinga dhidi ya maradhi hayo ambapo zoezi la chanjo linaendelea
kutolewa katika vituo mbali mbali vya Afya Mjini na Vijijini bila ya gharama
yoyote huku akiwaomba wajumbe wa baraza hili kuwahimiza wananchi katika majimbo
yao umuhimu wa chanjo hiyo kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya.
Pamoja na mambo
mengine, Hemed alizungumzia suala la
sensa ya watu na makaazi ambapo aliwataka viongozi na wanachi kwa ujumla
kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha zoezi hilo kutokana na
gharama kubwa zinazotumika katika kuendesha zoezi hilo.
Alisema kwamba, sensa
ya idadi ya watu na makazi ni jambo la msingi ambalo litasaidia kupanga vizuri
mipango ya maendeleo ya wananchi kwa miaka kumi ijayo kwa kupata takwimu halisi
na sahihi ya idadi ya watu na makaazi.
Katika sekta ya michezo,
Hemed alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi
imechukuwa jitihada za kutafuta wadhamini kwa ajili ya ligi mbali mbali kwa
msimu wa 2021/2022 ambapo utaanza hivi karibuni ambapo jumla ya fedha Millioni
Mia Tisa na Arobaini laki Tano na Elfu Kumi za Kitanzania zimechangishwa
(940,510,000/=)
Jumla ya miswada
mitatu imejadiliwa na kupitishwa ikiwemo, Mswada wa sheria ya kuanzisha Ofisi ya Mufti
Mkuu wa Zanzibar na kuweka usimamizi mzuri wa shughuli za kiislam Zanzibar, Mswada wa sheria ya
marekebisho ya Sheria mbali mbali na kuweka mashrti bora ndani yake.
Mswada wa sheria ya
kuanzisha Ofisi ya msajili wa Hazina na usimamizi wa mali za Umma na mambo
mengine yanayohusiana na hayo.
Baraza limeakhirishwa
mpaka siku ya Jumatano Disemba 15, 2021 saa Tatu Kamili za Asubuhi (3:00)
Mwisho.
0 Comments:
Post a Comment