Mkurugenzi TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa;Wanawake wanaposhiriki ipasavyo kwenye uongozi ni rahisi Nchi kupata maendeleo

 


Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akizungumza na waandishi wa habari 30 juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia.

Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akisistiza jambo kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye uongozi.



Makame Vuai Makame kutoka Tumbatu FM (katikati) akieleza kiasa ambacho alitumia chombo cha chake cha habari kupaza sauti na hatimae kupatikana kwa mabadiliko.


Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yanayotolewa na TAMWA-ZNZ kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ


Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi wa kisiasa na kijamii huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii za na Nchi kwa ujumla, kwani wanawake ni watu weye uwezo mkubwa na wepesi wa kutekeleza majukumu yao.

Dkt,Mzuri aliyasema hayo wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku 3 ya waandishi wa habari 30 wa vyombo mbali mbali Zanzibar kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia.

Alieleza kuwa Taifa lolote lile  haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo zaidi iwapo litawaacha wanawake nyuma na kuendeleza imani yakuwa  wanawake hawapaswi kuwa viongozi katika nyanja za kitaifa na hata kijamii.

Alisema licha ya   harakati mbali mbali zinazoendelea kufanyika visiwani Zanzibar kuhakikisha idadi kubwa ya wanawake wanashiriki kwenye uongozi bado hadi sasa hali hio haijaridhisha na wapo baadhi ya wenye nyadhifa au kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii wanaamini mwanamke hapoaswi kuwa kiongozi jambo ambalo si uhalisia.


Aidha Mkurugenzi huyo alifafanua na kwenda mbali zaidi kwa kueleza wapo baadhi ya watu kwa kutokuelewa wamekau wakitumia vipengele vya imani za dini kukandamiza wanawake wanapotaka kugombea kwenye uongozi licha ya kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwa viongozi na mitazamo hio ya dini haijamkataza mwanamke kuwa kiongozi.

 

Katika hatua nyengine alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya wanajamii kuendelea kuamini kuwa kushiriki kwa wanawake kwenye uongozi ni chanzo kikubwa cha uhuni huku wakisahau pia uhuni huo unaweza kufanywa hata na wanaume wanapokua kiongozi lakini kwa makusudi ya kuwachafua wanawake jamii imebeba taaswira hio potofu.


Awali mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo umelenga kuwafikisha wanawake elfu sita kutoka wilaya kumi na moja za Unguja na Pemba.


Alisema wanufaika wote wa mradi huo watajengewa uwezo dhidi ya ushiriki wa wanawake katika uongozi na umuhimu wa demokrasia.

Mradi huo wa miaka mine unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na ZAFELA pamoja na PEGAO chini ya ufhadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 Comments:

  1. Hongera sana Dkt. Mzuri na TAMWA hakika ushiriki na ushitikishwajj wa wanawake unaweza kutuvuusha na kufikia maendeleo endelevu na Jumuishi.

    ReplyDelete