| Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akizungumza na waandishi wa habari 30 juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia. |
| Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akisistiza jambo kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye uongozi. |
| Makame Vuai Makame kutoka Tumbatu FM (katikati) akieleza kiasa ambacho alitumia chombo cha chake cha habari kupaza sauti na hatimae kupatikana kwa mabadiliko. |
| Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yanayotolewa na TAMWA-ZNZ kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania. |
Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ
Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi wa kisiasa na kijamii huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii za na Nchi kwa ujumla, kwani wanawake ni watu weye uwezo mkubwa na wepesi wa kutekeleza majukumu yao.
Dkt,Mzuri aliyasema hayo wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku 3 ya waandishi wa habari 30 wa vyombo mbali mbali Zanzibar kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia.
Alieleza kuwa Taifa lolote lile haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo zaidi iwapo litawaacha wanawake nyuma na kuendeleza imani yakuwa wanawake hawapaswi kuwa viongozi katika nyanja za kitaifa na hata kijamii.
Alisema licha ya
harakati mbali mbali zinazoendelea kufanyika visiwani Zanzibar
kuhakikisha idadi kubwa ya wanawake wanashiriki kwenye uongozi bado hadi sasa
hali hio haijaridhisha na wapo baadhi ya wenye nyadhifa au kuwa na ushawishi
mkubwa kwenye jamii wanaamini mwanamke hapoaswi kuwa kiongozi jambo ambalo si
uhalisia.
Aidha Mkurugenzi huyo alifafanua na kwenda mbali zaidi
kwa kueleza wapo baadhi ya watu kwa kutokuelewa wamekau wakitumia vipengele vya
imani za dini kukandamiza wanawake wanapotaka kugombea kwenye uongozi licha ya
kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwa viongozi na mitazamo hio ya dini haijamkataza
mwanamke kuwa kiongozi.
Katika hatua nyengine alieleza kusikitishwa kwake na
baadhi ya wanajamii kuendelea kuamini kuwa kushiriki kwa wanawake kwenye
uongozi ni chanzo kikubwa cha uhuni huku wakisahau pia uhuni huo unaweza
kufanywa hata na wanaume wanapokua kiongozi lakini kwa makusudi ya kuwachafua
wanawake jamii imebeba taaswira hio potofu.
Awali mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir
Lusangi alisema mradi huo umelenga kuwafikisha wanawake elfu sita kutoka wilaya
kumi na moja za Unguja na Pemba.
Alisema wanufaika wote wa mradi huo watajengewa uwezo
dhidi ya ushiriki wa wanawake katika uongozi na umuhimu wa demokrasia.
Mradi huo wa miaka mine unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa
kushirikiana na ZAFELA pamoja na PEGAO chini ya ufhadhili wa Ubalozi wa Norway
Nchini Tanzania.
Hongera sana Dkt. Mzuri na TAMWA hakika ushiriki na ushitikishwajj wa wanawake unaweza kutuvuusha na kufikia maendeleo endelevu na Jumuishi.
ReplyDelete