Dr Shajak atoa shukrani zake kwa UNFPA

 


Katibu Mkuu wa Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akizungumza na nsaidizi mwakilishi mkaazi wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshuhulikia Idadi ya watu Duniani   (UNFPA)DKT. Wilifred Ochan Afisini kwake Migombani

Katibu Mkuu wa Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak na akizungumza na nsaidizi mwakilishi mkaazi wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshuhulikia Idadi ya watu Duniani   (UNFPA)DKT. Wilifred Ochan Afisini kwake Migombani


Raya Hamad – OMKR.

   

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar. D Shajak amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA kwa juhudi inazozichukuwa katika kusaidia Watu wenye Ulemavu.

 

 Ameeleza hayo ofisini kwake Migombani alipofanya mazungumzo na Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Dkt Wilfred Ochan kuhusiana na nafasi ya Watu wenye Ulemavu katika maendeleo ya nchi na kutoa shukurani kwa shirika hilo kwa kusaidia kuanzisha mfumo jumuishi wa Watu wenye Ulemavu.

 

Dkt Shajak amesema kuwepo kwa mfumo jumuishi wa Watu wenye Ulemavu umekuwa ni suluhisho katika kuisaidia Serikali kufanya maamuzi sahihi kwa vile unawezesha kujua idadi ya Watu wenye Ulemavu, aina ya ulemavu wao na kiwango chake pamoja na mahitaji yao.

 

Amesema mfumo jumuishi unaweka takwimu sahihi kufahamu ukubwa na udogo wa mahitaji ya Watu wenye Ulemavu na hatimae serikali kufanya maamuzi mazuri katika ya utekelezaji wa mipango yake kuanzia ngazi ya shehia hadi serikali kuu.

  

Aidha amesema pamoja na kuwepo kwa mfumo huo lakini bado unahitaji maboresho ili uweze kwenda mbali hivyo kupitia UNFPA anaimani wataweza kufikia malengo na watu wenye Ulemavu kupata stahiki zao zote ikiwemo kuwajengea uwezo kielimu, afya na ushiriki wao katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.

 

Nae Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Dkt Wilfred Ochan amesifu jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa juhudi wanazozichukuwa katika kuwasaidia Watu Wenye Ulemavu.

 

Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha masuala ya Watu wenye Ulemavu yanaendelea kutambuliwa na kuingizwa katika sera kwenye sekta mbali mbali kama vile afya, elimu, miundombinu shirikishi, makaazi na ajira ilikuwepo na ufanisi.

 

Kupitia UNFPA wameahidi kuendelea kufanya kazi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Watu wenye Ulemavu na kuona namna ya kufanya mashauriano katika mpango mkuu wa miaka mitano ujao ili kuyaingiza masuala ya Watu wenye Ulemavu yakiwemo masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea uwezo kielimu. .  

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment