DC Suzan akerwa na uchakavu wa vyoo SUZA kampasi ya Nkuruma


Na Abdalla Hemed Ali

ahemed@marhabanews.net

Uchakavyu wa majengo na huduma za choo zisizoridhisa katika kampasi ya Mkuruma chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA zinatajwa kuwa  changamoto kubwa zinazowakabili wanafunzi wanaosima katika kampasi hio.

Kutokana na uwepo wa changamoto hio Mkuu wa Wilaya ya Magharib A Unguja Suzani Kunambi alifika  katika eneo hilo na kuutaka uogozi wa chuo hicho kuhakikisha changamoto hio inatatuliwa haraka iwezekanavyo.

Alisema Serikali inatambua na kuthamini juhudi za wanafunzi hivyo kuna kila sababu wanafunzi hao kuwekewa mazingira mazuri ikiwemo huduma za nzuri za vyoo.

Kwa upande wake mtalamu wa maswala ya afya kutoka chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Dkt.Hamisa Juma  alisema ni wazi kuwa vyoo vya vinavyotumiwa na wanafunzi katika kampasi hio si rafika na havipaswi kutumiwa na wanafunzi.

Akizungumzia suala hilo mkuu wa kampasi ya Mkuruma Dkt,Haroun alisema anafahamu uwepo wa chanagmoto hio na tayari walishamkabidhi kazi hio mkandarasi lakini hadi sasa hawajui amekwama wapi.

Alisema hata hivyo katika kampasi hio kuna vyoo zaidi ya hamsini hivyo ni gharama kubwa kukarabati vyoo hivyo na nijambo linalopaswa kutazwa kwa upana zaidi.

 

 


About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment