![]() |
Katika hali isiokua ya
kawaida wala kutarajiwa na wengi katika medali za kisiasa visiwani Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF
Zanzibar Ndugu Abass Juma Muhunzi amemtaka Mwanyekiti wa chama hicho Prf,
Ibrahim Lipumba kujiuzulu katika nafasi hiyo mara moja kutokana kile alichokiita kushindwa kuitendea haki nafasi ikiwa ni
pamoja na kukiyumbisha chama hicho kwa upande wa Zanzibar.
Akizungumza na waandishi
wa Habari wa vyombo mbali mbali kisiwani Pemba Muhunzi alisema Mwenyekiti wa chama hicho amekuwa mtu wa
mwanzo anaevunja katiba ya chama hicho na kujichukulia sheria mikononi mwake kwa maslahi yake
binafsi bila kuangalia maslahi ya chama
hicho jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo katika chama.
Alisema CUF ni miongoni
mwa vyama vilivyoasisiswa kwa malendo maalumu ikiwa ni pampoja na kuwagomboa
wananchi kutokana na shida mbali mbali hivyo inapotokea Mwenyekiti kuvunja
katika ni sawa na kuipinga dhamira ya kuasisiwa chama hicho.
Alieleza kuwa njia pekee
ya kukinusuru chama hicho ni Mwenyekiti wa kuachia nafasi hio ili apishe
wengine ambao watakiongoza chama kwa misingi ya katiba.
Kwa upande wake Kaimu
Makamu mwenyekiti wa upande wa Zanzibar Mussa Haji Kombo alisema endapo mwenyekiti huyo ataendelea kubaki katika chama hicho chama kitazidi kupoteza hadhi yake kwa
wanachi kwa vile kiongozi huyo
anasababisha migogoro ya kila siku ndani ya chama hicho pamoja na kukikosesha
maslahi muhimu yakuendeshea harakati za
chama.
Alisema njia pekee ya
kukiendesha na kukiimarisha chama hicho ni Mwenyekiti kukaaa pembeni ili wenye
nia safi waendeshe chama.
Alisema Wanachama
wanapaswa kufahamu ukweli juu ya dhamira alionayo Mwenyekiti wao kwa sasa ni
pamoja na maslahi binafsi bila kuzingatia maslahi mapana ya walio wengi.
Kwa upande wake aliewahi
kuwa Naibu katibu mkuu Zazibar Ali Makame alisema kuendesha chama bila ya
kufuata katiba ni kwenda kinyume ambapo hukumu yake ni kuadhibiwa.
Alisema kwa muda mrefu
mwenyekiti wao amekua akiendesha chama bila kufuata katiba na kupelekea mgawanyiko
mkubwa kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara
Mkutano huo wa waliokua
viongozi wa CUF ulijumlisha viongozi mbali mbali wapatao 34 kutoka maeneo
tofati ya kusini na kaskazini Pemba.

0 Comments:
Post a Comment