![]() |
| Makamu wa kwanza wa Rais Wa Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman |
Ameyasema hayo katika kikao maalumu pamoja na viongozi wa ACT Wazalendo wa mikoa yote saba ya kichama ya kisiwani Unguja kilichofanyika kwenye Ukumbi Wa Majid Hall, uliopo Kiembe Samaki, Magharibi ‘B’ Unguja.
Aidha, amesema ni muhimu kuendelea kujenga hoja madhubuti, nidhamu pamoja na uwajibikaji kama misingi ya kukiendeleza chama hicho.
Sambamba na hayo, amewakumbusha wanachama hao kuendelea kudumisha amani ya kweli na uwajibikaji kwa lengo la kuinua maendeleo ya Zanzibar.
Mapema Kiongozi wa ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe, amesema Chama hicho kitaendelea kuhakikisha makubaliano yaliyopo baina yao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yanatekelezwa ikiwemo suala la uchunguzi juu ya waathirika wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, uwepo wa tume ya maridhiano itakayotoa haki sawa kwa raia wote pamoja na kuwepo kwa chaguzi za haki nchini.
Kikao hicho kimekamilisha ziara ya viongozi wa chama hicho iliyoanza tarehe 9 Agosti huko kisiwani Pemba, ambapo kwa ujumla wamekutana na viongozi wa Mikoa 11 ya kichama, Majimbo 50 pamoja na Matawi 682 ya chama hicho kwa Unguja na Pemba.

0 Comments:
Post a Comment