Katika hali isiokuwa ya kawaida wala kutarajiwa na wapenzi wa soka Nchini Tanzania aliewahi kuwa msemaji wa timu ya Simba na sasa ni msemaji wa timu ya Yanga Haji Sunda Manara amewahuskuru wapenzi wa timu hio kumpokea kwa shangwe kubwa la aina yake.
Manara alitoa kauli hipo katika kilele cha siku ya wananchi ilifanyika jijini Dar Es Salama na kueleza kuwa hakuwa hipata hamasa na shauku kama hio kwa miaka yote.
Hata hivyo Manara alitumia sehemu hio kwa kujiuliza ni kwanini Baba yake alikubali yeye kwenda simba wakati yanga ndio timu ambayo ina hamasa kubw ana kumpa furaha.
Manara akiwatambulisha wachezaji wa Yanga kabla ya kuanza mechi, amesema msimu huu Yanga ni ya Makombe na sio vingine.
Katika tukio la kipekee, Manara alimfunga kamba za viatu Kiungo mahiri wa Yanga Feisal Salum ‘ Fei Toto’ na kumsifia kwa uwezo wake mkubwa uwanjani.
Aidha, katika sherehe hizo zilizomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Zanako, Yanga iliwatumia wachezaji wake wapya na kuangalia tathmini ya kila mmoja.
Kwenye mchezo huo Yanga imekubali kichapo cha goli 2-1 goli kwa upande wa Yanga likifungwa na Heritier Makambo.

0 Comments:
Post a Comment