Milango imefunguliwa wanawake jitokezeni muwe viongozi:Dkt,Mzuri



Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akionesha msisitizo wa jambo kuhusu umuhumu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi wakati wa uwasilishwaji wa ripoti maalumu ua utafiti huo.

Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania, Zanzibar ( TAMWA-ZNZ) Dkt. Mzuri Issa amesema mazingira ya kisiasa Nchini Tanzania hivi sasa yanatoa fursa kwa wanawake wengi kuwa viongozi wa Serikali na taasisi binafsi kufuatia Nchi kuongiozwa na Rais Mwanamke ambae ni  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa Chama hicho uliopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja wakati alipokua akizungumza na viongozi mbali mbali kutoka vyombo vya habari na wawakilishi wa asasi za kiraia.

Kauli hiyo ya Mkurugenzi Dkt Mzuri imekuja kufuatia uwasilishwaji wa ripoti maalumu iliyolenga kuona ni kwa kiasi gani baadhi ya vyombo vya habari vinavyoandika habari za wanawake katika nafasi za uongozi visiwani Zanzibar.

Alisema kwa mazingira yaliopo hivi sasa ni wazi kuwa Nchi imefunguka na fursa zaidi za wanawake walio wengi kuwa viongozi na wanachopaswa ni kujidhatiti na kuwa tayari kugombea nafasi hizo.

Akifafanua zaidi Dkt. Mzuri alisema ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi si jambo la kuonekana kuwa kikwazo bali ni matakwa ya dunia yenye dhamira ya kuleta usawa kwa watu wote hivyo hakuna sababu kuona mwanamke kutoshiriki katika nafasi za uongozi.

Sambamba na hayo alitoa wito kwa jamii hususani wanandoa kuacha dhana potofu yenye lengo la kumkandamiza mwanamke kutokua kiongozi kwa madai ya baadhi ya wanandoa kuamini  wanawake wanapokua viongozi hubadilika na kukataa ndoa zao za awali.

Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo aliwataka viongozi wa vyombo vya habari Zanzibar  kuhakikisha wanatoa kipaombele zaidi kwa habari za wanawake, pamoja na kuwa na sera maalumu itatakayowawezesha waandishi wa habari kuandika habari za mambo mazuri yaliyofanywa na wanawake wengi viongozi katika majumu yao ya kila siku.

Awali akiwasilisha ripoti hiyo ya utafiti mkufunzi wa masuala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alisema utafiti huo mdogo ulijikita katika kuangalia magazeti mawili ambayo ni gazeti la Mwananchi na gazeti la Zanzibar Leo.

Alisema kuna uhaba wa habari za wanawake na uongozi, zikiwemo za wanasiasa katika magazeti ambayo yamefanyiwa utafiti huo wa miezi minne ambao uliangalia magazeti ya mwezi Febuari, April, Juni na Agasti 2021.

Akifafanua zaidi alisema katika habari 159 za gazeti la Zanzibar Leo zilizotolewa na kuwahusu wanasiasa ni asilimia 25.16  ndizo zilizowagusa wanawake moja kwa moja na kwa upande wa gazeti la Mwananchi katika habari  180 zilizotolewa na kuwagusa wanasiasa  ni asilimia 46.1 tu ndizo zilizogusia viongozi na wanasiasa wanawake.

Sambamba na hayo Dkt, Abuu alieleza kuwa kuonekana kwa idadi kubwa zaidi katika gazeti la Mwananchi ni kwa sababu ya kumuandika Rais Samia lakini viongozi wengine wanawake hawakupata nafasi kubwa.

Alisema kupitia utafiti huo ni wazi kuwa kuna tatizo kwenye vyombo vya habari la kukutoa fursa zaidi kwa wanawake jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na wasimamizi wa vyombo hivyo ili kubadili mtazamo na kutoa fursa zaidi kwa sauti za wanawake viongozi kwenye vyombo vyao.

Akichangia uwasilishwaji wa ripoti hiyo Mwenyeki wa wanaume wa mabadiliko Mohamed Jabir alisema  vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuwaandika wanawake kwani wao ndio watu ambao wanakabiliana na changamoto kubwa katika harakati za kisiasa na uongozi,sambamba kujikita katika habari zinazohusu wanasiasa na viongozi chipukizi.

Kwa upande wake mhariri wa Gazeti la Zanzibar Leo Ramadhan Makame alisema wameuchukua utafiti huo kama changamoto na kuahidi kuzifanyia kazi na anaamini utafiti kama huo ukifanyika tena mwakani basi utakua na matokeo mazuri zaidi juu ya sauti za wanawake na uongozi.

 

Maelezo ya Picha.

 

01.Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akionesha msisitizo wa jambo kuhusu umuhumu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi wakati wa uwasilishwaji wa ripoti maalumu ua utafiti huo.

02.Mhariri mtendaji wa shirika la magazeti ya Serikali Ali Haji Mwadini akisisitiza jambo alipokua akichangia ripoti hio katika ukumbi wa TAMWA ,Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

03.Mwandishi wa habari wa kituo cha Zenj FM radio Jumanne Ramadhani akieleza umuhimu wa wahariri kuwasaida waandishi hususani katika habari za takwimu.

 

04.Mkufunzi wa maswala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alipokua akiwasilisha ripoti hio huku akisislizwa kwa makini na washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi mbali mbali.


Mkufunzi wa maswala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alipokua akiwasilisha ripoti hio huku akisislizwa kwa makini na washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi mbali mbali.

Mwandishi wa habari wa kituo cha Zenj FM radio Jumanne Ramadhani akieleza umuhimu wa wahariri kuwasaida waandishi hususani katika habari za takwimu.

Mhariri mtendaji wa shirika la magazeti ya Serikali Ali Haji Mwadini akisisitiza jambo alipokua akichangia ripoti hio katika ukumbi wa TAMWA ,Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

About mmedia

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment